Site icon Soko Directory

Mashetani Wekundu Watisha, Huku Arsenal Ikitoka Sare

By Antonney Oduor

Mashetani wekundu waliicharaza klabu kutoka uhispania Real Sociedad mabao manne kwa bila jawabu mjini Turin, uwanjani Allianz.

United ilianza kampeni yake vizuri baada Bruno Fernandes kufunga mawil, Marcus Rahford na Daniel James kufunga orodha ya wafungaji hao.

Hii inaipatia vijana hao wa Ole Gunner nafasi nzuri ya kufuzu katika awamu ya kumi na sita bora. Mechi ya marudiano itachezwa wiki ijao alhamisi usiku.

Washika Bunduki wa Arsenal walitoka sare ya kufunga mabao moja Na Benfica Ya Ureno. Benfica walitangulia kufunga kupitia mkwaju wa penalti. Bao lililotiwa kimyani na mshambuliaji wao Pizzi. Arsenal wakajibu mapigo dakika mbili baadae kupitia winga wao Bukayo Saka na kuhakikisha bado Gunners bado wana matumaini ya kufuzu katika awamu hiyo ya kumi na sita bora.

Arsenal walikuwa na nafasi nyingi kumaliza mchezo huo lakini walikosa nafasi za wazi huku nahodha wao kuomba msamaha kwa nafasi alizozitupa nje na kuhahidi kwamba atatia bidi kwa mechi ya marudio ili wapate tiketi ya kufuzi katika hatua nengine.

Matokeo mengine ni kwamba Ranger walitoka na ushindi wa mabao manne kwa moja dhid ya wapinzani wao Antwerp. Olympiacos iliilaza PSV  mabao manne kwa mawili. AS Roma wakainyuka Braggaa mabao mawili kwa nunge. Ac Milan wakatoka sare ya mabao mawili na FK Crvena Zvezda. Tottenham wakaichraza Wolfsberger mabao manne kwa moja. Mechi za marudiano zitashuhudiwa wiki ijayo.

Kule nchini Uingereza ni kwamba wikendi hii kutakuwa na mechi za kusisimua mno. Ijumaa ya leo Wolves wataikaribisha Leeds Unites ugani Molineaux usiku wa saa tano. Kesho Southampton wataikaribisha Chelsea pale St. Mary’s. Everton itakuwa wageni wa Liverpool pale Anfield alafu Jumapili Arsenal watawaalika vinara wa ligi Manchester City pale Emirata. United itacheza na Newcastle pale Old Trafford.

Usikkose kutazama mechi hizi kwani zitakuwa na mvuto si haba. Tupilia mbali kaski ya ndovu kumfanya mwanae kitoweo kule jangwani.

About Author

A freelance  Journalist Who has much interest in sports and trends. He says it as it is and brings out the bitter truth and the thrill in the game.

 

Exit mobile version