Site icon Soko Directory

Chelsea Yatia Guu Moja Robo Fainali, Bayern Kutetea Taji Lao

By Antonney Oduor

Yaliyotarajiwa hayakufanyika kule Roma. Kijana kutoka Ufaransa Olivier Giroud alifunga bao la kipekee katika dakika sitini na nane na kuweza kuipatia Chelsea ushindi wa bao moja bila mtungi dhidi ya vinara wa La Liga Atletico Madrid.

Ilidhaniwa Wahispania wataibuka na ushindi lakini juhudi ziliambulia patupu kwani Mkufunzi wa Chelsea Thomas Tuchel alionyesha ubabe wake wa michuano hii. Hii inaifanya The Blues kupatwa nafasi murwa ya kufuzu katika awamu nyengine ya michuano haya.

Bingwa Mtetezi Byaern Munich walizidi kutetea taji lao barani ulaya baada ya kutitiga Lazio Ya Uitaliano mabao manne kwa moja kwenye mechi ambayo inakisiwa Wana wa Naples walikuwa nyumbani.

Mabao hayo yalitiwa kimyani na mshambuliaji wao Robert Lewanowski, Leroy Sane, kinda wao  Jamal Musial na la mwisho ilikuwa bao la kujifunga kupitia mchezaji wa Napoli Francesco Acerbi. Wana hao wa Bravarians wanapigiwa upato mkubwa sana kufika robo fainali na kuzidi kutetea taji hilo.

Leo mabingwa mara kumi na tatu katika michuano hii Real Madrid wataalikwa na Atalanta pale Gewiss Bergamo. Real madrid walibanduliwa katika awamu hii msimu uliopita na wana matumaini ya kwamba wanaeza kutoa nuksi dhidi ya Atalanta.

Atalanta wameshinda mechi mbili katika ya tatu ya michuano hii msimu huu kujipatia nafasi mwafaka ya kufuzu katika kumi na sita bora. Real Madrid watakosa huduma za wao kama Karim Benzema, Dani Carvajal, Eden Hazard, Marcelo, Alavaro Odriozola,  Rodrygo Federico Valverde na Sergio Ramos.

Baada ya kuchapwa na Mainz wikendi iliyopita Borrusia Monchegladbach hawana fomu nzuri Sanaa baada ya kupoteza mechi mbili, sare mbili na ushindi mmoja katika michuano haya na ni mara yao ya kwanza kufuzu katika awamu ya kumi na sita bora.

Na pia hawajawai kushinda katika michuano mmine iliyopita dhidi ya wababe wa Ulaya. Huku Manchester City wana msururu wa mechi kumi na nane bila kupoteza mechi na la kushangaza ni kwamba hawajawai kuwa nyuma katika mechi kumi na saba walizocheza na wapinzani wao. City wameshinda mechi nne dhidi ya wapinzani kutoka ujeruamani. Mechi hiyo itachezwa ugani Puskas Arena, Budapest.

Usikose kufuatilia mechi hizi leo jioni ukitamani kuwa rah asana tupilia mbali ya kibogoyo kuota magego na sagego ya kutafunia ubwabwa.

Exit mobile version