Site icon Soko Directory

Kivumbi Cha Ligi Ya Mabingwa Ya Barani Ulaya

By Antonney Oduor

Mbiu yam gambo ikilia hivyo basi lazima kuwe na dharura. Siku ya leo itakuwa kaski ya ndovu kumla mwanae. Kule barani ulaya kutashuhudiwa mechi kali baina ya Atletico Madrid na Chelsea. Mechi ambayo itachezwa ugani Arena Nationala Bucharest saa tano usiku.

Atletico ni  wanaongoza jedwali kule La Liga na wanapigiwa upato mkubwa sana kuliinu taji hilo. Wana hao wa Diego Sineone wana nafasi nzuri ya kushinda mechi hiyo. Mabao za Atletico huwa zimekuja katika dakika za majeruhi. Na katika na tisa ya michuano haya Atletico wameshinda sit ana imekuwa dhidi ya wababe wa Ulaya.

Chelsea bado wana rekodi nzuri ya kutopigwa chini ya Mkufunzi Thomas Tuchel. Katika mechi ya juzi ndipo walikuwa wamefungwa katika kipindi cha kwanza na Southampton lakini baadae walijizatiti na kufanya mambo yatoke sare baada ya mkwaju wa adhabu kutoka kwa Mason Mount. Mechi ya leo itakuwa ya kusisimua mno kwani kila mtu atatafuta ushindi katika awamu hii ya kwanza.

Mabingwa watetezi wa michuano hii Byaern Munich leo watakaribishwa na Lazio kutoka kule uitaliano ugani Stadio Olimpico, Rome katika mechi ambayo Bayern inataka kuendeleza rekodi yao nzuri ya ushindi. Lazio bado hawajapoteza mechi yeyote barani ulaya na wanapania kuendeleza rekodi yao nzuri ya kutopigwa mechi kumi mfululizo. Katika ya mechi hizo ambazo wameshinda wamekuwa wakiongoza katika kipindi cha kwanza.

Bayern waemkosa kupata ushindi katika mechi dhidhi ya Frankfurt wikendi iliyopita baada ya kulazwa mabao mawili kwa moja wamekuja kuonyesha ubaya wao huko Roma. Cirro Immobile ndo atakuwa mchezaji wa kutisha uwanjani leo kwani amefunga mabao yake mengi chini ya dakika thelathini huku Kingsley Coman amefunga mabao mawili kati ya mechi tatu alizocheza.

Uingereza ni kwamba Leeds wataikaribisha Southampton pale Elland Road katika mechi yao ya bakshihi. Leeds wamekuwa na ushindi mzuri siku ya Jumanne katika mechi ambazo wamecheza. Huku Southampton inatafuta ushindi wao wa kwanza tangu Januari nne.

Usikpse kutamaza mechi leo usiku kwani ladha Zaidi ya kitoweo ya nyama.

About Author

A freelance  Journalist Who has much interest in sports and trends. He says it as it is and brings out the bitter truth and the thrill in the game.

Exit mobile version