By Antonney Oduor
Mabingwa wa ufaransa PSG waliigaraza mabingwa wa uhispania Barcelona mabao manne kwa moja ugani Nou Camp, jana katika mechi ya kusimumua iliyoshuhudiwa na maelfu ya watu waliokuwa wameisubiria kwa hamu ghamu usiku wa kuamkia leo.
Lionel Messi alifungua ukarasa wa mabo kupitia adhabu ya mkwaju wa penalti katika dakika ya 25 pale ambapo De Jong alichezewa ndivyo sivyo. PSG ilijibu mapigo wakisawazisha katika dakika ya thelathini na moja kupitia mshambuliaji wao Kylian Mbappe ambaye alifunga mabao matatu na kuisaidia timu yake kuwa na asilimia kubwa kufuzu katika awamu ya robo fainali. Mose Keane alifunga bao moja na kuifanya mabao nne na kuikata matumaini ya wanakatalunya kukomboa mabao hayo.
Hii ni mara ya pili mchezaji mmoja kufunga mabao matatu dimbani camp nou baada Andrey Shevchenko ambae alikuwa wa kwanza kufunga mwaka wa 1997 akiwa na timu ya Dyniamo Kiev. Matokeo haya yanamweka mkufunzi wa Barcelona Ronald Koeman katika kuti kikavu kwani timu yake ya Barcelona huenda wakabanduliwa katika michuano haya mapema kama ilivyotarajiwa. Ikumbukwe kwamba wafaransa wa PSG walikosa huduma za staa wao Neymar Junior. Je unadhani Bareclona wataeza kufuzu katika awamu yar obo fainali baada ya kudhalilishwa nyumbani?
Liverpool pia wana nafasi nzuri ya kufuzu katika raundi nyengine baada ya kuicharaza RB Leizpig mabao mawili sufuri. Shukran kwa wachezaji wawili Saidio Mane na Mohammed Salah walioweza kuibuka na ushindi huo. Licha ya matokeo yao duni kule uingereza vijana hao wa Jurgen Klopp walijikakamua ili kunusurika na ushindi.
Leo Mabingwa wa italia Juventus wataalikwa katika uga wa Estadio do Dragao huko ureno na kilabu ya Porto ili waweze kuminyana nao huku Borrusia wataalikwa na Sevilla huko uhispania kuchuana katika awamu ya kumi na sita bora. Mechi zote zitachezwa mwendo was aa tano usiku.
About the author
A freelance Journalist Who has much interest in sports and trends. He says it as it is and brings out the bitter truth and the thrill in the game.
