By Antonney Oduor,
Bao La El Arabi halikutosha kuipeleka Olympiacos katika awamu Ya Robo fainali baada ya Kuzidiw kete na washika Bunduki wa Arsenal ambao kule ugenini walikuwa na Mabao matatu.
Arsenal ilijaribu kuweka mambo yawe Sawa ugani Emirata ila dakika zilikuwa zimekatika ugani. Arsenal walifuzu licha ya sheria za mabao za ugenini. Mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta alionyesha kugadhabishwa sanaa na suala hilo.
Kwengineko Kule Zagreb tulishuhudia Spurs Ya Mourinho kubanduliwa na Dinamo Zagreb ambae kocha wao anatumikia kifungo cha miaka minne kwa kosa la jinai. Hiyo haiwakifisha Tamaa wana Dinamo Kwani walitoka nyuma kuilima Tottenham mabao matatu kwa nunge na kutolewa katika michuano hizo.
Ac Milan, Rangers na Young boys pia walifuata Mkondo baada ya kubanduliwa na Manchester United ambae Pogba alifunga bao la kipekee, Slavia Prague ambao walishinda bao la kipekee na Ajax Kama ifuatavyo.
Droo ya michuano haya yatafanywa huko Nyon kujua hatima ya robo fainali. Wikendi hii kutakuwa na mitafaruku Ya mechi ya Ligi na Za Fa. Arsenal watacheza Ligi baada ya kubanduliwa FA .
Arsenal itacheza na Westham kule London Stadium, Aston Villa watacheza na Tottenham huku Leeds ikicheza na Southampton. Manchester United watacheza Fa Na Leicester huku Manchester City watacheza na Everton, Sheffield watacheza na Chelsea
Wikendi yenye hanjam kubwa sanaa. Usiachwe nyuma
