Na Antonney Oduor
Timu ya Harambee stars ilitoka na wajukuu wa Farao katika wa michezo ya Kasarani hapo jana kwa mabao moja kwa moja. Wamisri hao walitanguli kufunga bao katika dakika ya pili kupitia mshambuliaji wao Mohammed Magdi Kafsha baada ya Abdalla Hassan kuweka mambo kuwa sawa katika dakika ya sitini na tano.
Johnstone Omurwa alikatisha tamaa ya Harambee kuongeza bao la pili baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu. Na mwishowe mechi kutoka sare. Kenya wanapaswa kuwapiga Togo ndiposa wafuzu katika michuano ya Afcon barani Afrika mwaka ujao.
Pierre Emerick Aubameyang aliisaidia nchi yake ya Black Panthers, Gabon katika michuano ya kikombe barani Afrika baada nchi yake ya kuigaragaza nchi ya Demokrasia ya Congo mabao matatu kwa nunge. Zimbwabwe waliibuka na ushindi baada kuitinga Botswana bao moja bila jawabu.
Taifa ya stars ya Tanzania wakafungwa na Equitorial Guinea, Tunisia kuwafanyia makuruhu Libya baada ya kuwachapa mabao matano kwa mawili na hatimae Aljeria kutoka sare ya mabao matatu kwa matatu na Zambia.
Katika mechi ya kufuzu ya Kombe la dunia, nchi ya Uingereza iliichapa San Marino mabao matano kwa nunge, James Ward Prowse, Calvert Lewin mabao mawili, Sterling na Ole Watkins yalitosha timu hiyo three lions kutoka na ushindi kule ugani Wembley.
Ujerumani hawakuachwa nyuma baada ya kuwafundisha wana wa Iceland mabao matatu kwa nunge, Ikay Gundogan, Khai Havertz na Leon Goretzka walikuwa wafungaji wa washindi hao wa dunia mwaka 2014. Uhispania ikatoka sare na Wagiriki, Sweden kufunga Georgia bao moja kwa nunge. Amazuri wa uitaliano hawakuwasamehea North Ireland baada ya kuwafunga mabao mawili kwa nunge.
Wikendi hii tutazidi kushuhudia mechi za nchi kadhaa wa kadha kwani wiki nayo hakuna mechi za ma vilabu.
