Site icon Soko Directory

Koeman Akalia Kuti Kikavu, Klopp Apata Faraja

Wababe wa uhispania Barcelona walibanduliwa katika michuano ya ligi ya mabingwa ulaya na miamba wa ufaransa Paris Saint Germain.

By Antonney Oduor

Wababe wa uhispania Barcelona walibanduliwa katika michuano ya ligi ya mabingwa ulaya na miamba wa ufaransa Paris Saint Germain kwa jumla ya mabao matano kwa mawili. Jana mechi yao ilienda sare ya moja kule Paris katika uga wao wa Parc De Princess. Bao la psg lilifungwa na mshambuliaji wao rai wa kifaransa Klyian Mbappe kupitia mkwaju wa penalty huku mshindi wa Balon d’or mara tano Lionel Messi aliweka mambo yakwa sawa lakini baadae akakosa mkwaju wa penalti kuiweka Barcelona mbele. Vivyo hivyo inakisiwa kwamba Mkufunzi wa Barcelona huenda akafutwa kazi iwapo hatabeba kikombe msimu huu ikiwa veterani wao Xavi Hernandez huenda akapewa kazi baada ya rais mpya kuteuliwa hivi majuzi.

Kule Budaqest, Liverpool walipata ushindi wa mabao mawili bila jawabu. Mabao hayo yalifungwa na Mohamed Salah na Saidio Mane. RB Leizpig ilibanduliwa kwa jumla ya mabao manne kwa nunge. Licha ya matokeo mabaya kwenye ligi ya uingereza huku ulaya wameonyesha ubabe wao kwa kufuzu awamu yar obo fainali. Matokeo hayo yalimfurahisha Kocha wako Jurgen Klopp baada siku kadhaa zilizopita kulikuwa na matokeo mabaya.

Kule uingereza ni kwamba vinara wa ligi kuu, Manchester City waliwavurumishia hasira vijana kutoka Mtakatifu Maria Southampton mabao matano kwa mawili. Mabao hayo yalifungwa na Kevin De Bruyne na Ryard Mahrez wote kufunga mawili huku mjerumani Ikay Gundogan kufunga lake moja. Mabao ya Soton yalifungwa na James Ward-Prowse kupitia penalty na Chei Adams. Cityzens sai wako kileleni na alama sitini na nane. Pep Guardiola alifurahishwa na matokeo hayo baada wikendi kufungwa na mahasimu wao Manchester United.

Kule Uhspania katika michuano ya La liga, vinara wa ligi Atletico Madrid walikata matumaini ya Athletico Bilbao baada ya kuifunga mabao mawili kwa moja. Mabao ya Madrid yalifungwa na Marcos Llorente huku Luis Suarez akiongeza la pili kupitia mkwaju wa penalty. Bao la Bilbao lilifungwa na Iker Muniain. Atletico Madrid sai wanaongoza jedwali wakiwa mbele na alama sita Zaidi ya wapinzani wao Barcelona na majirani Real Madrid.

Exit mobile version