By Antonney Oduor
Bao la kipekee la Diogo Jota lilihakishia Liverpool ushindi katika uwanja wa Molineux, Wolverhampton. Bao hilo lilifungwa katika ziada kabla mechi hiyo haijaenda mapumzikoni baada ya kupokea pasi murwa kutoka kwa msenegali Saidio Mane.
Wolves wajizatiti kutafuta bao katika kipindi cha pili lakini juhudi zao ilikuwa kama kupigia mbuzi gitaa. Kwani walinzi na mlinda wa Liverpool walikita kambi na kutokubali makosa yeyote yatokee. Huu ni ushindi wa kwanza wa Liverpool baada kupoteza mechi sita mfululizo pale Anfield. Hii inaifanya Liverpool kuruka hadi nafasi ya sita katika jedwali la ligi kuu uingereza.
Lionel Messi alihakikisha kwamba orodha ya mabao yake yanafika ishirini na moja kusaidia timu yake ya Barcelona kupanda hadi nafasi ya pili katika jedwali la liga baada ya kuititiga Huesca mabao manne kwa moja. Antione Griezmann a Oscar Mingueza walihakikisha kwamba wacatalunya hao wanatoka na alama tatu muhimu.
Bao la Huesca lilifungwa kupitia mkwaju wa penalty na Rafael Mir Vicente. Hii inaifanya Barca kuwa nyuma ya Athletico Madrid na alama nne na mbele ya Real Madrid na alama mbili.
Ziada:
Kule Barani Ulaya ni kwamba leo kutakuwa na karamu ya ndovu kumfanya mwanae chamcha wakati mechi za marudiano ya awamu ya kumi na sita bora mkondo wa pili. Manchester City watacheza na Borussia Monchengladbach kule ugani Puskas Arena. Kwenye mechi ambayo wana wa Pep wako kifua mbele na mabao mawili kwa nunge. Inakisiwa kwamba City wanapigiwa upato wa kuendeleza rekodi ya kuvuka katika awamu ya robo fainali.
Kwengineko ni kwamba Real Madrid wataialika Atalant katika uga wao wa Alfredo Di Stefano huko Uhispania kucheza katika mkondo wa pili wa awamu hii. Real wanaongoza mechi hiyo na bao moja tu huku wakisaka nafasi ya kufuzu katika awamu nyengine ya robo fainali. Wana hao wa Los Blancos wako na majeruhi kama yafuatayo: Dani Carvajal, Casemiro, Eden Hazard, Mariano na Odriozola. Lakini wana matumaini makubwa kupata ushindi wa leo.
