Site icon Soko Directory

Matokeo Ya Kufuzu Katika Kombe La Dunia

FKF

Na Antonney Oduor

Mabingwa wa duniani wa mwaka wa 2018, Ufaransa walifunga nchi ya Kazakshtan mabao mawili kwa nunge katika mechi iliyochezwa mjini Paris. Mabao ya Ufaransa Yalifungwa na Ousmane Dembele na lengine wapinzani hao wakajifunga.

Uingereza walijikatia Tiketi yao ya kucheza Kombe la Dunia baada kuuonyesha ubabe wao waliinyuka Albania mabao mawili kwa nunge. Harry Kane na Mason Mount walikuwa wafungaji wao.

Nahodha wa Armenia Henrikh Mhkitaryan aliisaidia nchi yake kushinda dhidhi ya wapinzani wao Iceland kwa mabao mawili kwa nunge.

Dernmak ikaaichapa Maldova mabao nane bila jawabu. Ushindi huo ulikuwa mkubwa sanaa kwa Wadenish hao tangu nchi iyo iwe na waanzilishi.

Pau Torres na Alvaro Morata waliisaidia Uhispania kuicharaza Georgia mabao mawili kwa Moja.

Austria ikaaichapa Faore islands mabao matatu kwa Moja. Bulgaria wakapoteza dhidhi ya Waitaliano huku Wana Israeli wakapata sare dhidi ya waskoti.

Sweden wakailaza Kosovo mabao matatu kwa nunge.

Uswizi nao pia wakaifunga Lithuania bao Moja bila jibu. Bao la kipekee kufungwa na Shaqiri mshambuliaji wa Liverpool. Poland wakaifunga Andorra mabao matatu kwa nunge, na pia ujerumani kuifunga Romania bao Moja bila jawabu.

Huku Afrika Ni Kwamba,

Namibia walifunga Guinea mabao mawili kwa moja, Taifa Stars ya Tanzania wakapata bao Moja dhidi ya Libya, Watunisia wakaandikisha ushindi wa mabao mawili kwa moja, huku Ghana wakailaza Sao Tome and Principe na hatimaye Susan kuilaza Afrika Kusini kwa mabao mawili kwa nunge.

Exit mobile version