Site icon Soko Directory

Real Na City Wajikatia Tiketi, Chelsea Bayern Guu Moja Ndani

Betika

Antonney Oduor

Mabingwa wa Ulaya mara kumi na tatu Real Madrid walijiandikisha ushindi wa mabao matatu kwa moja dhidi ya Atalanta ya uitaliano na kujifanya kufuzu katika awamu ya robo fainali.

Mabao ya Wana Los Blancos hao Yalifungwa na Karim Benzema, Sergio Ramos na Marco Asensio huku La Atalanta likifungwa na Muriel katika dakika za lala salama. Hii iliifanya Real Kufuzu na jumla ya mabao manne kwa moja ukijumuisha awamu ya kwanza na ya pili.

Madrid inakuwa timu ya kwanza kutoka Uhispania Kufuzu katika awamu ya Robo fainali baada Ya Barcelona na Sevilla kubanduliwa.

Kwengineko ni Kwamba the Citizens waliwashambulia Borussia Monchengdlabach mabao mawili kwa nunge na kuifanya City Kufuzu katika Mkondo wa babe bora Ulaya. Mabao hayo Yalifungwa na Kevin De Bruyne huku Ikay Gundogan alibatilisha msumari wa mwisho katika Jeneza la wajerumani hao. Hii inaifanya city kuwa timu ya kwanza kutoka uingereza Kufuzu katika awamu nyengine huko Ulaya. Matokeo yanawapa nguvu Kwani Vinara hao wa uingereza wanapigiwa sana upato kulitwaa taji hilo.

Ziada;

Kwengineko ni Kwamba kule Stamford Bridge kutakuwa na kivumbi, Kwani wababe wawili kutoka pale tofauti za Ulaya watakuwa wanashuka pale Stamford Bridge kuminyana hii ni Kati ya Athletico Madrid na Chelsea. Chelsea Wanaenda katika mechi wakiwa na bahati ya kupata bao la ugenini dhidi ya Athletico. Wahispania hao ambao wataongozwa na Luis Suarez katika safu Ya Ushambuliaji watategemea sana huduma Za Mchezaji huyo.

Kwengineko ni Kwamba Bayern pia watanuia kufika katika awamu za robo fainali wakitaka kuendeleza rekodi yao nzuri dhidi ya Napoli kutoka Italia baada ya awamu ya kwanza kutoka na ushindi mzuri.

Usikose kutazama mechi hizo Kwani zitakuwa za furaha ghaya kibogoyo aliyeota magego na sagego angalau ya kutafuniwa ubwabwa kaski ya Iddi.

Exit mobile version