Site icon Soko Directory

Tuchel Azidi Kutoa Mafunzo, Bayern Wafuzu

By Antonney Oduor

Chelsea ilifuzu awamu ya Robo fainali baada ya kuibadua Athletico Madrid kwa jumla ya mabao matatu kwa nunge kiujumla. Hii ni mara ya kwanza tangu mwaka wa 2014. Mabao hayo Yalifungwa na Hakim Ziyech huku Emerson kijana kutoka uitaliona kusukuma msumari wa mwisho alipoingia na kugusa mguso wake wa kwanza.

Tuchel anakuwa mkufunzi wa kwanza kuitoa na kuchapa Athletico katika awamu zote mbili bila kuwa na Mchezaji mahiri Cristiano Ronaldo. Matokeo haya yanaifanya Chelsea kuwa timu ya tatu kutoka uingereza Kufuzu baada ya Manchester City na Liverpool kujikatia tiketi zao Hapo awali.Tuchel anakuwa kocha kocha wa kwanza kutofungwa baada ya mechi kumi na tatu alizocheza, Kwani ameshinda tisa, kutoka sare nne na kutofungwa hata moja.

Kwengineko ni Kwamba Choupo Mouting na Lewandowski waliisaidia Bayern kucharaza Lazio kwa mabao mawili kwa moja. Hii imesaidia Wana hao wa Braverians Kufuzu pia katika awamu hizo za robo fainali. Hii inaifanya Bayern Kufuzu katika awamu hii mara ya kumi na tisa mfululizo. Droo za robo fainali zitafanyika ijumaa  ya kesho kujua mchuano huo utachukua Mkondo Gani.

Ziada: Chelsea Yatia Guu Moja Robo Fainali, Bayern Kutetea Taji Lao

Leo katika Michuano ya Europa Ni Kwamba Arsenal itataka Kufuzu katika Mkondo wa robo fainali baada ya kupata mabao matatu kule Athens Juma liliopita.Leo watacheza katika uga wao wa Emirata kuhakikisha ya Kwamba wamefuzu.

Manchester United wataalikwa ugani San Siro Kupambana na Ac Milan ambao Wana bao la ugenini walilolifunga wakiwa Old Trafford wiki iliyopita. Leo Ac Milan watapata huduma Za Mchezaji wao matata Zlatan Ibrahimovic  huku Manchester United watakuwa na Pogba na Cavani.

Ranger wataalia Slavia Prague,Zagreb wataalika Tottenham, Granada kusafiri kucheza na Molde, Villarreal kucheza na Kyiv, Shaktar Donestk kucheza na As Roma na hatimaye Young Young Boys kucheza na Ajax leo usiku.

Usikose kushuhudia uhondoo wa mechi hizo leo usiku.

Exit mobile version