Na Antonney Oduor
Mabao ya Marcus Rashford na Bruno Fernandes yalitosha kuipa uishindi Manchester United katika awamu ya Robo fainali dhidi ya Wapinzani wao kutoka Uhispania Granada.
United waliibuka na ushindi wao mabao mawili kwa nunge na kuwapa nafasi nzuri ya Kufuzu katika awamu ya nusu fainali. Hii inatokana na Manchester United na mabao mawili ya ugenini. Mechi ya marudiano itachezwa wiki ijayo Alhamisi na Vijana hao wa Ole Gunnar watakosa huduma Za Harry Maguire na Scott.
Arsenal walizembea dakika za mwisho na kuifanya Slavia Praha kusawazisha bao katika dakika za lala salama. Mechi Hiyo ilikuwa nuksi si haba baada ya Mbrazili Willian na Mfaransa Lacazette kugonga mlingoti mara mbili.
Bukayo Saka alikosa nafasi ya mwaka ili kuipa Arsenal ushindi wa mapema lakini ilibidi mashabiki wangoje hadi dakika ya themanini na sita ndo Nicolas Pepe kufungua ukurasa wa mabao.
Slavia hawakukata tamaa hadi kipenga cha mwisho na hatimaye kukomboa bao hilo. Mechi Hiyo Imekuwa ngumu sanaa kwa Arsenal Kwani watakuwa na mlima wa kupanda.
Villarreal ya Unai Emery walichapa Zagreb bao Moja kwa nunge. Bao hilo la kipekee lilifungwa na Gerard Moreno kutokana na Mkwaju wa Penalti.
Na.mwshowe Ajax walichapwa na Roma mabao mawili kwa Moja.
Na kule Uingereza ni Kwamba usiku wa leo Fulham watacheza na Wolves katika uga wa Craven Cottage.
Na msisahau wikendi hii kutakuwa na mechi kubwa ya El Clasico! RealĀ Madrid watapambana na Mahasimu wao jadi Fc Barcelona.
