By Antonney Oduor
Wanasema nyuki hutoa asali tamu basi mchezo wa kandanda hutoa utamu zaidi ya asali. Leo michuano ya ligi ya mabingwa ulaya itang’oa nanga usiku katika ynyanja mbalimbali.
Mabingwa wa ulaya mara tano Barcelona watawaalika wababe wa Ufaransa Paris Saint Germain (PSG) katika dimba lao la Camp Nou katika awamu ya kumi na sita bora kwenye michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya saa tano usiku.
Barcelona ambayo imekuwa rekodi nzuri katika kufuzu katika awamu ya robo fainali maana katika misimu kumi na minne ambayo wamejipata katika awamu ya kumi na sita wamefuzu zote.
Hii ni rekodi nzuri kwa wana Catalunya hao kwani mara ya mwisho wababe hao kupatana na mabingwa wa Ufaransa PSG waliicharaza mabao sita kwa moja mnamo mwaka wa 2017.
PSG watakosa huduma za staa wao wa kibrazili Neymar Junior ambaye anauguza jeraha la goti huku Angel Di Maria pia akiuguza majeruhi. Hii ni pigo kubwa sana kwa PSG ambao watakosa huduma za wachezaji hao. Bareclona watakosa huduma za Philipe Coutinho ambaye ameuguza jeraha la goti kwa muda mrefu. Huenda mchezaji wao mkongwe Gerrard Pique akarudi uwanjani leo kusakata dimba hilo.
PSG wamekuwa na rekodi mbaya ya kufuzu katika awamu ya robo fainali isipokuwa msimu uliopita dunia ilishuhudia wakifika fainali na kocha wao aliyekula kalamu Thomas Tuchel. Hiyo ilikuwa mara ya kwanza katika historia yao.
Je, PSG wamekuja kulipiza kisasi cha mwaka wa 2017 au Barcelona watajizatiti kuitetea rekodi yao? Basi hapo mida ya saa tano usiku tutajua kati ya Simba na Chui nani mfalme wa jangwani.
Kule ujerumani miamba wa Uingereza Liverpool watacheza katika uwanja wa Puskas Arena (Budapest) ambao wanasema ni ‘neutral stadium’ kutokana na janga la corona na RB Leipzig. Msimu uliopita wajerumani walishangaza watu sana baada ya kufika nusu fainali baada ya kubanduliwa na PSG.
Liverpool wamekuwa na rekodi mbaya sana katika michuano ya Uingereza baada ya kupoteza mechi tatu mfululizo. Mabingwa hao wa ulaya kwa mara ya sita wamekuwa ma mikosi ya majeruhi kupelekea matokeo ya duni uwanjani. Ikumbukwe kwamba kocha wao Jurgen Klopp alifiliwa na mamake mzazi huko ujerumani na katika mahojiano jumapili alisema hilo halitamtatiza uwanjani kwani ni Maisha tu.
Usikose kushuhudia mechi ya mabingwa ulaya kwani kuna uhondo mkubwa tupilia mbali kaski ya ndovu kumfanya mwanawe kitoweo.
About the author
A freelance Journalist Who has much interest in sports and trends. He says it as it is and brings out the bitter truth and the thrill in the game.
