Skip to content
Entertainment

Haya Hapa Matokeo Ya Kufuzu Katika Kombe La Dunia 2022

BY Soko Directory Team · March 25, 2021 07:03 am

KEY POINTS

Jumatano kulikuwa na mechi kadha wa kadha kuwania nafasi za Kufuzu katika Mchuano mkubwa wa kidunia la kombe la dunia wa mwaka 2022.

Na Antonney Oduor

Jumatano kulikuwa na mechi kadha wa kadha kuwania nafasi za Kufuzu katika Mchuano mkubwa wa kidunia la kombe la dunia wa mwaka 2022.

Uturuki iliigaragaza Uholanzi mabao manne kwa mawili. Mshambuliaji wa Lille Burak Yilmaz alifunga mabao matatu huku kiungo mshambuliaji wa Ac Milan Hakan Calhanoglu kufunga moja na kufanya matokeo kuwa manne. Wadachi walijikakamua kufufua matumanini yako lakini juhudi zao ziligonga tu mwamba. Walibahatika kurudisha mabao mawili tu kupitia Davy Klaassen na Luuk De Jong huku Memphis akakosa mkwaju wa penalti katika dakika za lala salama.

Wabelgiji waliandikisha ushindi mzuri baada ya vijana hao Wa Roberto Martinez ya kuipa adabu Wales kwa mabao matatu kwa moja.

Kevin De Bruyne, Thogan Hazard na Mkwaju wa Penalti wa Romelu Lukaku ilitosha kuwapa wabelgiji hao tabasamu mioyoni mwao. Wales walipata bao la kufutia machozi kupitia Harry Wilson.

Mabingwa wa Dunia mwaka wa 2018, Ufaransa walitoka sare ya bao moja moja na Ukraine kule jijini Paris. Wafaransa hao walitangulia kufunga bao kupitia mshambuliaji wao Mchezaji wa Barcelona Antoine Griezman baada Ya Presnel Kimpembe kujitia Kati lango lao na kuifanya Ukraine kutokuwa na kazi ya ziada na mechi Hiyo kutoka sare.

Slovenia ilistaajabisha dunia baada ya kuitinga Croatia bao moja bila jawabu. Bao hilo LA kipekee lilifungwa na Sandi Lovric.

Urusi nae pia haikuachwa nyuma kwa kutoka na ushindi dhidi ya wapinzani wao Malta Kwa mabao matatu kwa moja.matokeo mengine ni Kwamba Ureno ilishinda bao moja kwa nunge dhidi ya wapinzani wao Azerbaijan. Serbia ikailaza Ireland mabao matatu kwa mawili, Norway ikaibuka na ushindi wa mabao matatu kwa nunge dhidi ya Gilbratar, Bosnia ikatoka sare na Finland na huku Czech Waliifundisha Estonia kabumbu baada ya kuwanyuka mabao masita kwa mawili.

Na huku kwetu katika bara la Afrika kutakuwa na mechi kadha wa kadha ya Kufuzu katika michuano Ya Afcon. Katika wa Uga wa Kasarani Hapa mjini Nairobi, Harambee Stars wataminyamana na wajukuu wa Farao katika uga wa Kasarani. Misri waliingia mjini siku Ya Jumanne ili kuchuana na Kenya ambao wanakosa huduma Za nahodha wao Victor Wanyama. Hii inamaanisha Micheal Olunga atashikilia nafasi ya unahodha Leo jioni wakati wamisri hao watakuwa na huduma Za mshambuliaji wao Mo Salah na wachezaji wengine kama akina Elneny na El Ghazi. Itakuwa kipute kikubwa sana.

Mechi zengine ni Kwamba Afrika kusini watacheza na Ghana, Zambia na aljeria, Gabon kuchuana na DRC Congo huku Taifa Stars Ya Tanzania Kucheza na Guinea.

Soko Directory is a Financial and Markets digital portal that tracks brands, listed firms on the NSE, SMEs and trend setters in the markets eco-system.Find us on Facebook: facebook.com/SokoDirectory and on Twitter: twitter.com/SokoDirectory

Trending Stories
Related Articles
Explore Soko Directory
Soko Directory Archives