Haya Hapa Matokeo Ya Kufuzu Kwa Kombe La Africa

KEY POINTS
Harambe stars ya Jacob Ghost Mulee ilisafiri hadi Togo katika uga wa Stade De Kegue huko Lome kuandikisha ushindi wa mabao mawili kwa Moja.
Na Antonney Oduor
Harambe stars ya Jacob Ghost Mulee ilisafiri hadi Togo katika uga wa Stade De Kegue huko Lome kuandikisha ushindi wa mabao mawili kwa Moja. Kenya ilitangulia kufunga bao katika dakika ya thelathini na tatu kupitia Mchezaji wa Bandari Fc Hassan Abdala.
Kenya walionyesha umahiri wao na baadae katika dakika ya hamsini na tano Masoud Abdala akaweka la pili kupitia mkwaju wa penalti. Togo walijaribu kukaza kamba na juhudi zao zikafua dafu pale ambapo walipata bao la kufutiwa machozi kupitia Mchezaji wao Henri Eninful katika dakika za lala salama. Hii inaifanya Togo na Kenya wote kukosa nafasi ya Kufuzu katika Kombe la barani Afrika.
Wamisri nao waligadhabishwa na matokeo ya kutoka sare hivi majuzi pale Kasarani na kumimina hasira zote kwa Comoros baada ya kuwachapa mabao manne bila jawabu. Mohammed Elneny alifungua ukurasa wa mabao katika dakika ya kumi saba badae Mohammed Sheriff kuongea la pili. Maji yaliwazidi Wana Comoros unga ikabidi tusonge Ugali hakuna Tena kupika uji wa mtama, Mohamed salah akatia mawili na kuikatisha Tamaa Comoros ambao tayari walikuwa washafuzu.
Kule Angola nao pia waliwastaabisha Dunia baada ya kuichapa Gabon mabao mawili kwa nunge. Gabon ambao nahodha wao Aubaemayang ambae tayari alikuwa amerudi kule London kujiunga na kikosi cha Arsenal hakucheza mechi iyo ambao nchi yake tayari ilikuwa ishafuzu katika michuano hayo.
Chipolopolo ya Zambia iliwachapa Zimbwawe mabao mawili kwa nunge kule Harare katika mechi ya kusisimu mno.
Mabingwa watetezi wa kombe hilo.la Africa Aljeria iliwapa Botswana kipigo cha mbwa kutabasaki msikitini baada ya kuwanyorosha mabao matano kwa nunge.
Huku Demokrasia Ya Jamhuri ya Congo ilipata ushindi wao wa kwanza dhidi Ya Gambia kule Kinshasa kwa bao Moja tu. Mwishowe ni Kwamba Burkina Faso waliandikisha ushindi wao dhidi ya Sudani Kusini kwa bao Moja kwa nunge.
Leo Ivory Coast watacheza na Uhabeshi, Nigeria itacheza na Lesotho huku Cameroon watacheza na Rwanda.
About Soko Directory Team
Soko Directory is a Financial and Markets digital portal that tracks brands, listed firms on the NSE, SMEs and trend setters in the markets eco-system.Find us on Facebook: facebook.com/SokoDirectory and on Twitter: twitter.com/SokoDirectory
