Real Madrid Watoka Sare, Everton Waibuka Na Ushindi

KEY POINTS
Bao la dakika ya mwisho ya Vinicius Junior ilisaidia Real Marid kupata alama moja katika yao ya ishirini na tano La Liga katika mechi walikuwa wanacheza na Real Sociedad.
By Antonney Oduor
Bao la dakika ya mwisho ya Vinicius Junior ilisaidia Real Marid kupata alama moja katika yao ya ishirini na tano La Liga katika mechi walikuwa wanacheza na Real Sociedad.
Mechi hii imehaibu msururu wa Real Madrid kwa ushindi wao mechi tano mfululizo. Sociedad waliokuwa waliotangulia kufunga bao hilo katika kipindi cha pili ya dakika hamsini na tano kupitia mchezaji wao Portu baada ya kupokea pasi murua kupitia Nacho Monreal.
Hii inaifanya Real Madrid kushikilia nambari ya tatu na alama hamsini na tatu huku Barcelona na Atletico Madrid wakiwa mbele yao jedwalini.
Bao la mapema katika dakika za mwanzo wa mchezo kupitia Richarlison ilipatia Everton ushindi mwembamba dhidi ya Southampton ambao bado wanatafuta ushindi wao wa kwanza tangu Januari nne. Southampton walijitahidi lakini juhudi zao ziligonga mwamba.
Bao la Micheal Keane lilikataliwa na sheria za VAR aambazo zingendeleza ushindi wao. Jordan Pickford alifanya jitihada sana pasiingie bao dakika ya tamati. Hii inaiweka Everton katika nafasi ya saba na alama arubaini na tatu huku Southampton wakishikilia nafasi ya kumi na nne na alama thelathini.
Huku kwengine ni kwamba vinara wa ligi kuu uingereza Manchester City wataikarbisha Wolves leo usiku ili kuendeleza ushindi wao wa Zaidi ya mechi ishirini wa kuliteta taji lao huu msimu. Wolves wamekuwa ambao mechi iliyopita walifungwa na Newcastle wanajaribu kutoka na ushindi dhidhi ya Vinara wa ligi.
About Soko Directory Team
Soko Directory is a Financial and Markets digital portal that tracks brands, listed firms on the NSE, SMEs and trend setters in the markets eco-system.Find us on Facebook: facebook.com/SokoDirectory and on Twitter: twitter.com/SokoDirectory
