Juventus Wabanduliwa Ligini, Dortmund Wafuzu

KEY POINTS
Licha ya Juventus kushinda mechi ya jana ambayo ilienda hadi muda wa ziada. Hawakuwa na nafasi ya kuendeleza kampeni zao katika nafasi yar obo fainali.
By Antonney Oduor
Licha ya Juventus kushinda mechi ya jana ambayo ilienda hadi muda wa ziada. Hawakuwa na nafasi ya kuendeleza kampeni zao katika nafasi yar obo fainali. Mabao mawili ya Federico Chiesa yaliisaidia Juventus kufikishana na Fc Porto katika muda wa ziada ila mabao ya mawili ya wareno hao iliifanya Juventus kubanduliwa katika michuani hayo.
Porto walipewa kadi nyekundu katika dakika za mapema lakini bidi zao za mchwa kujenga kichuguu kwa mate iliifanya wafuzu katika raundi ya robo fainali. Andre Pirlo alionekana kugadhabishwa na matokeo hayo. Porto ilifuzu na mabao ya ugenini ambayo ni sheria ya michuano haya.
Kule Ujeruma ugani Signal Iduna, Borussia Dortmund walifuzu baada ya kutoka sare ya mabao mawili kwa mawili. Mabao mawili ya Erling Haaland yalifanikisha wajerumani hao kufuzu na Zaidi ya mabao matano ukijumuisha na yale ya mkondo wa kwanza dhidi ya wapinzani wao kutoka uhispania Sevilla, anbayo inasemekana hawajawi fuzu Zaidi ya raundi ya kumi na sita bora.
Leo PSG watashuka dimbani Parc des Princess kuchuana na Barcelona ambayo katika awamu ya kwanza Psg iliichapa wanacatalunya hao mabao manne kwa moja kule Camp Nou. Barcelona wataenda kujaribu kufufua matumaini yao ya kufuzu katika awamu ya robo fainali. Mechi hiyo itakuwa ngumu kwani Psg wanapigiwa upato kulibeba taji hilo la ulaya. Wafarsnsa watakosa huduma za mchezaji wao mahiri Neymar Junior na Moise Keane huku Barca ikikosa huduma za Gerard Pique, Ansu Fati, Philipe Coutinho na Sergio Roberto.
Liverpool wataccheza na RB Leipzig ugani Puskas Arena Budapest. Mechi ambayo Liverpool wanaongoza kwa mabao mawili. Leizpig watanuia kujiendeleza katika michuano hayo. Huku Liverpool wakiwa ma fomu mbaya kwa ligii kuu ya uingereza. Wachezaji wanaotiliwa shaka kucheza mechi ya leo ni Roberto Firmino na mcezaji wao mpya Kabak kutokana na majeraha.
Kule uingereza ni kwamba Manchester City watarudi kutetea taji lao leo wakishuka ugani Etihad kupambana na Southampton. Vinara hao watarudi kuendeleza msururu wao ushindi katika ligii kuu hiyo.
About Soko Directory Team
Soko Directory is a Financial and Markets digital portal that tracks brands, listed firms on the NSE, SMEs and trend setters in the markets eco-system.Find us on Facebook: facebook.com/SokoDirectory and on Twitter: twitter.com/SokoDirectory
