Skip to content
Entertainment

Ole Gunnar Kukalia Kiti Kikavu, Leicester Wafuzu

BY Soko Directory Team · March 22, 2021 11:03 am

KEY POINTS

Matumaini ya mashetani wekundu kutwa taji lolote msimu huu unanzidi kudidimia kwani jana katika uga wa King Power walipewa kichapo cha mbwa kutabasaki msikitini.

By Antonney Oduor

Matumaini ya mashetani wekundu kutwa taji lolote msimu huu unanzidi kudidimia kwani jana katika uga wa King Power walipewa kichapo cha mbwa kutabasaki msikitini baada kupewa mabao matatu kwa moja katika awamu ya robo fainali katika michuano ya FA.

Mabao ya The Foxes ilifungwa mhezaji mahiri kutoka Nigeria Kelechi Iheanacho ambae alifunga mabao mawili na Youri Tielemans kufunga moja. Manchester United walipata bao la kufutia machozi kupitia Mason Greenwood. Chelsea pia ilijipatia tiketi ya nusu fainali baada kuibandua Sheffield kwa mabao mawili kwa nunge.

Hakeem ziyech aliendeleza tena rekodi yake ya mabao baada kufunga la pili huku la kwanza Sheffield kujitia wenyewe. Vinara wa ligi kuu uingereza Manchester City walifika nusu fainali baada ya kuibandua Everton kwa mabao mawili kwa nunge shukran kwa mabao ya Kevin De Bruyne na Ikay Gundogan.

Mechi za nusu fainali itakuwa katika ya Chelsea na Manchester City huku Southampton wakipambana na Leicester Aprili kumi na saba mwaka huu.

Ligii kuu uingereza ni kwamba Arsenal walitoka nyuma na kutoka sare ya mabao matatu kwa tatu na Westham United katika mechi iliyokuwa ya kusisimua sana baaada ya Arsenal kuwa nyuma katika dakika thelathini za kwanza. Jesse Lingard,  Jarrod Bowen na Thomas Soucek waliiweka wana nyundo hao kifua mbele baaada ya westham kujifunga mabao mawili huku Lacazette kuokoa jahazi katika kipindi cha lala salama. Tottenham nao pia walirudisha hasira za kubanduliwa katika michuano ya Europa baada ya kuicharaza Aston villa mabao mawili kwa nunge. Carlos Vinicius na Harry Kane walikuwa wafungaji wao katika mechi ya jana.

Vinara wa ligii kuu ya Ufaransa PSG walicharaza Lyon mabao manne kwa mawili ambapo Kylian Mbappe alieka mawili huku Di Maria na Danilo kufunga moja. Mabao ya Lyon yalifungwa na Cornet na Slimani. Matokeo haya yanaifanya PSG kushika usukani tena katika ligi hiyo baada siku za nyuma walikuwa wanashika nafasi ya tatu..

Mabao mawili ya Lionel Messi na mawili ya Sergino Dest yaliifanya Barcelona kuicharza Real Sociedad mabao sita kwa moja. Mabao mengine ya wakatalunya hao yalifungwa na Griezmann na Dembele. Messi kwa sasa amefunga mabao ishirini na tatu katika ligi kuu ya la liga.

Soko Directory is a Financial and Markets digital portal that tracks brands, listed firms on the NSE, SMEs and trend setters in the markets eco-system.Find us on Facebook: facebook.com/SokoDirectory and on Twitter: twitter.com/SokoDirectory