Skip to content
Entertainment

Matokeo Ya Kufuzu Katika Kombe La Dunia Mwaka 2022

BY Soko Directory Team · March 31, 2021 09:03 am

KEY POINTS

Wanasema Mbiu Ya Mgambo ikilia hivyo basi kuna jambo. Hapo Jana katika viwanja mbali tulishuhudia matokeo kadha wa kadha huku baadhi ya nchi kutoka Ulaya kuonyesha ubabe wao.

Na Antonney Oduor

Wanasema Mbiu Ya Mgambo ikilia hivyo basi kuna jambo. Hapo Jana katika viwanja mbali tulishuhudia matokeo kadha wa kadha huku baadhi ya nchi kutoka Ulaya kuonyesha ubabe wao.

Ubelgiji iliamua hasira si hasara baada ya kuwafanya Belarus kitoweo hapo katika uga wa Den Dreef ( Hervelee) baada ya kuipa Belarus kichapo cha mbwa kutabasaki msikitini ya mabao nane kwa nunge.

Uholanzi nao walitiwa Mori na kusema wataendeleza ushindi wao mabao mengi baada ya kuichapa Gibraltar mabao saba kwa bila jawabu. Luka Modric aliongoza Croatia kutoka na ushindi wa mabao matatu kwa nunge.

Ureno Ya Cristiano Ronaldo iliibuka na ushindi wa mabao matatu kwa Moja dhidi ya Luxembourg baada Diogo Jota, Ronaldo na Paulinha kufunga mabao hayo.

Norway walitoka kule Montenegro na ushindi mwembamba wa bao Moja kwa nunge. Slovakia pia walikuwa kipau mbele kuwadhibiti Urusi baada ya kuwagaragaza mabao mawili kwa Moja.

Uturuki itoka sare na Na Latvia Mabao matatu kwa matatu.Jamhuri ya Czech ilipewa kichapo na Wales baada Ya Daniel James wa Manchester United kufunga bao hilo LA kipekee katika kipindi cha lala salama.

Kule Afrika ni Kwamba Ivory coast waliinyuka Uhabeshi mabao matatu kwa nunge na kujikatia tiketi ya Kufuzu katika michuano ya Kombe la Barani Afrika.Morrocco walijitahidi sanaa tupilia mbali mchwa kujenga kichuguu kwa.mate baada ya kuing’o Burundi bao Moja kwa nunge.Carpe Verde wakawanyorosha Mozambique bao Moja kwa nunge, Cameroon wakatoka sare tasa na Rwanda, wasenegali watoka sare ya bao Moja Moja na Eswatini kule Afrika Mashariki Nigeria wakailaza Lesotho kwa mabao matatu kwa nunge na hatimaye Mauritania wakaichapa Afrika Ya Kati  bao Moja bila usemi.

Mechi za Nchi kadha wa kadha zinaelekea kufika kikomoni kwani baadhi ya wachezaji tayari washaanza kurudi katika vilabu vyao Ulaya.

Soko Directory is a Financial and Markets digital portal that tracks brands, listed firms on the NSE, SMEs and trend setters in the markets eco-system.Find us on Facebook: facebook.com/SokoDirectory and on Twitter: twitter.com/SokoDirectory

Trending Stories
Related Articles
Explore Soko Directory
Soko Directory Archives