Skip to content
Entertainment

Pep Abatizwa Na Moto Pale Etihad Na Mashetani Wekundu

BY Soko Directory Team · March 8, 2021 11:03 am

KEY POINTS

Wahenga walisema kilicho na mwanzo hakikosi mwisho. Hatimaye rekodi nzuri ya Manchester City ya kutofungwa katika mechi ishirini.

By Antonney Oduor

Wahenga walisema kilicho na mwanzo hakikosi mwisho. Hatimaye rekodi nzuri ya Manchester City ya kutofungwa katika mechi ishirini na moja mfululizo ilifika ukingoni baada ya Mashetani wekundu kuwatoa sadaka siku tukufu ya Jumapili.

Manchester United walifungua ukurasa wa mabao kupitia mkwaju wa penalty ambapo Bruno Fernandes alipachika wavuni katika dakika za mwanzo wa mchezo. Luke shaw alitia msumari wa mwisho katika sanduku la City na kuiteketza matumaini yao na kutoka ushindi nyumbani kwao. City bado wanaongeza jedwali wakiwa mbele na alama kumi na moja Zaidi.

Liverpool imeshindwa kupata ushindi ugani Anfield katika mechi sita walizocheza mwaka huu. Hii ni rekodi mbaya Sanaa tangu mwaka wa 1951/1952 walipokuwa na rekodi hiyo. Jana katika uga wao Fulham ilitoka na ushindi mwembamba dhidi yao baada ya Mario Lemina kufunga bao maridadi dakika chache kabla waelekee mapumzikoni. Ilikuwa bao ya kwaza Fulham kufunga ugani Anfield tangu mwaka wa 2006 baada ya Martin Skertel kujifunga mwaka huo. Masaibu ya Liverpool yamepamba moto ikisiwa kwamba huenda Kocha wao Jurgen Klopp kujiuzulu.

Mechi zengine zilizochezwa ni kwamba Tottenham walicharaza Crystal mabao manne kwa moja huku Gareth Bale na Harry Kane wote wakifunga mawili kila mooja. West Brom na Newcastle walitoka sare ya kutofungana. Arsenal pia ilitoka sare ya bao moja kwa moja.

Kule Uhispania Real Madrid na Atletico Madrid walitoka sare ya kufungana bao moja. Mabao hayo yalifungwa na Luis Suarez na Karim Benzema. Barcelona pia iliicharaza Osasusana mabao mawili kwa nunge. Hayo yanajiri huku Barcelona wameamua kuchagua rais wao mpya wa club Joan Laporta baada ya kushinda uchaguzi uliofanyika jana kule Catalunya. Zoezi hilo ilikuwa ya muhimu sana kwani hata wachezaji wakongwe walikuja kufanya zoezi la uzalendo.

Leo kutakuwa na mechi kati ya Chelsea na Everton huku Westham wakiikaribisha Leeds United pale London Stadium.

Soko Directory is a Financial and Markets digital portal that tracks brands, listed firms on the NSE, SMEs and trend setters in the markets eco-system.Find us on Facebook: facebook.com/SokoDirectory and on Twitter: twitter.com/SokoDirectory

Trending Stories
Related Articles
Explore Soko Directory
Soko Directory Archives