Skip to content
Entertainment

Tuchel Azidi Kuonyesha Ufundi Wake, Mount Amnusuru

BY Soko Directory Team · March 5, 2021 11:03 am

KEY POINTS

Wana wa Blues walizidi kuonyesha umahiri wao chini ya mkufunzi wao mgeni Thomas Tuchel ambae alipata kibarua chake Januari mwakani. 

By Antonney Oduor

Wana wa Blues walizidi kuonyesha umahiri wao chini ya mkufunzi wao mgeni Thomas Tuchel ambae alipata kibarua chake Januari mwakani. Katika ya mechi saba alichocheza kocha huyo hajapoteza mechi yeyote ila kutoka sare mbili tu. Jana katika dimba la Anfield Chelsea waliandikisha ushindi wao wa kwanza ndani ya miaka sita ugani hapo.

Bao la kipekee lililofungwa na muingereza Mason Mount katika kipindi cha kwanza mnamo dakika ya arubaine na mbili hii ni baada kupokea pasi murwa kutoka kwa Ngolo Kante. Liverpool walijaribu kuweka mambo sawa lakini mlinda lango wa Chelsea alikuwa ange sana kuhakikisha wametoka na alama zote tatu.

Bao la wana wa Tuchel ambalo Timo Werner kulifunga lilikataliwa na sheria za VaR na kusema kwamba alikuwa amejenga kibanda katika ardhi ya wenyewe. Ushindi huu inaifanya Chelsea kukaa katika nafasi ya nne huku Liverpool kushuka hadi nafasi ya saba.

Jose Mourinho aliandikisha ushindi mwengine baada ya timu yake Tottenham kupata ushindi mwembamba wa bao moja kwa nunge. Bao hilo la kipekee lililofungwa mchezaji wa Fulham kwa kujifunga katika dakika ya kumi na tisa lilofungwa na mcezaji Abdul-Nasir-Adarabioyo. Bao hilo lilitosha kupatia Spurs ushindi na alama tatu muhimu. Kwa sai vijana hao wa Mourinho wanashikilia katika nafasi ya nane na alama arubaini na mbili.

Carlo Ancelotti nae pia hakuachwa nyuma kwa kuzoa alama zake tatu muhimu. Everton pia walinusurika kupata ushindi huo mwembamba kupitia bao la kipekee la raia wa kibrazili Richarlison katika kipindi cha lala salama. Wana wa Toffees waliwazidi wapizani wao Westbrom kwa kete na hatimae kuibuka na ushindi huo.

Wikendi hii kutakuwa na kivumbi katika uga tofauti kwani Manchester city wataialika mahasimu wao wa jadi maeshetani wekundu katika uga wa Etihad. Mechi hiyo inajulikana kama ‘Manchester Derby’. Washika bunduki wa Arsenal watakuwa wageni wa Burnley pale Turf Moor. Fulham watasafiri hadi kule Anfield kupambana na Liverpool huku Brighton watacheza na Leicester kule Amex na Aston Villa watacheza na Wolves pale Villa Park.

Soko Directory is a Financial and Markets digital portal that tracks brands, listed firms on the NSE, SMEs and trend setters in the markets eco-system.Find us on Facebook: facebook.com/SokoDirectory and on Twitter: twitter.com/SokoDirectory

Trending Stories
Related Articles
Explore Soko Directory
Soko Directory Archives