Skip to content
Entertainment

Ukuta Wa Kigiriki Wangushwa Na Washika Bunduki

BY Soko Directory Team · March 12, 2021 01:03 pm

KEY POINTS

Arsenal iliendeleza rekodi yake nzuri kutofungwa ulaya. Hii inaipa Arsenal upao mbele ambao wanapigiwa upato kulitwaa taji la Europa msimu huu.

Mabao ya Martin Odegaard, Gabriel Maghallaes na Mohammed Elneny yalitosha kuubomoa ukuta wa wagiriki kutoka Athens. Arsenal iliendeleza rekodi yake nzuri kutofungwa ulaya. Hii inaipa Arsenal upao mbele ambao wanapigiwa upato kulitwaa taji la Europa msimu huu.

Washika bunduki hao wana nafasi nzuri ya kufuzu katika raundi ya robo fainali baada ya kuwa mabao matatu ya ugenini. Beki wao wa zamani Sokratis ambae alikuwa anapiga kelele za chura kabla ya mechi alibaki kinywa wazi baada kuona klabu yake ya zamani kuigaragaza Olympiacos mabao matatu kwa moja ugani kwao Athens,

Mashetani wekundu walitoka sare na wababe wa italia Ac Milan ugani Old Trafford ya bao moja moja. Bao la kipekee la United lilifungwa na Amad Diallo katika dakika hamsini baada ya kupokea pasi mufti kutoka kwa Bruno Fernandes. Ac milan walitia juhudi zao za mchwa kuweka mambo yawe katika dakika za lala salama baada ya Simon Kjaer kutia kimyani na kupata la ugenini.

Mabao mawili ya muingereza Harry Kane yalitosha kuiweka Tottenham mbele dhidi ya wapinzani wao Dianamo Zagreb katika kule London.

Granada iliifunga Molde mabao mawili kwa nunge huku Villareal ya Unai Emery kuadabisha Dyn Kyiv. Ajax waligaragaza young boys mabao matatu kwa nunge. As roma kukata matumaini ya Shaktar Donetsk baada ya kuilaza mabao matatu kwa nunge huku Slavia Prague na Rangers wakatoka sare, mechi za marudiano zitachezwa wiki ijao alhamisi.

Wikendi hii kutakuwa na mechi ya mahasimu wa jadi kutoka London, huku Arsena wataikaribisha Tottenham katika uwanja wao wa Emirata. Manchester United watacheza na West ham, Leeds watashuka kuminyana na Chelsea, Manchester city watacheza na Fulham ugani Craven Cottge.

Soko Directory is a Financial and Markets digital portal that tracks brands, listed firms on the NSE, SMEs and trend setters in the markets eco-system.Find us on Facebook: facebook.com/SokoDirectory and on Twitter: twitter.com/SokoDirectory

Trending Stories
Related Articles
Explore Soko Directory
Soko Directory Archives