Skip to content
Entertainment

United Yatoka Sare, Liverpool, City Na Arsenal Washinda

BY Soko Directory Team · March 1, 2021 11:03 am

KEY POINTS

Manchester United walitoka sare tasa na magwiji wa London Chelsea katika mechi ilikuwa ya kusisimua mno.

By Antonney Oduor

Liverpool ilipata ushindi wake wa kwanza baada kupoteza mechi nne mfululizo. Curtis Jones na Roberto Firmino waliibuka kidede na kuipatia klabu ushindi wa mabao mawili kwa nunge dhidi ya vibonde wanaoshika nafasi ya mwisho katika jedwali la ligi kuu. Hii inaifanya Liverpool kuendelea kusihika nambari ya sita huku Westham na Chelsea wakiwa juu yao.

Manchester United walitoka sare tasa na magwiji wa London Chelsea katika mechi ilikuwa ya kusisimua mno. Chelsea walikosa nafasi za wazi kwani bahati yao ilikuwa haijasimama tisti kabisa. Hii inaifanya Chelsea kurudi hadi nambari tano na alama arubaini na nne. Huku United wakiwa na alama hamsini wakizdiwa na alama na kumi na mbili na majirani wao Manchester City.

Arsenal nao hawakuwachwa nyuma kwa kujizolea alamu tatu muhimu baada ya kuicharaza Leicester mabao matatu kwa moja. Leicester ambao wanashikilia nambari ya tatu jedwalini na alama arubaini na tisa walitangulia kufunga bao katika dakika ya sita kupitia mchezaji Youri Tielemans raia wa ubelgiji katika dakika ya sita. Washika bunduki walijibu mapigo baada ya David Luiz kufunga  katika dakika ya thelathini na tisa. Alexandre Lacazette alifunga la pili kupitia mkwaju wa penalti dakika moja kabla ya mapumziko huku Nicolas Pepe akakata matumaini ya Leicester kuibuka na ushindi.

Tottenham Hotspurs waliibuka na ushindi wa mabao manne bila jawabu dhidi ya Burnley. Mabao hayo yalifungwa na Gareth Bale ambae alifunga mawili huku Harry Kane na Lucas Moura wakaongeza mengine. Hii inaifanya Spurs kushikilia namba nane jedwalini.

Fulham walitoka sare tasa na Crystal Place, Newcastle walitoka sare ya bao moja na Wolves. Leeds walichapwa bao moja komboa ufe na Aston Villa huku Westbrom walichapa Brighton bao moja kwa nunge baada ya Danny Welbeck na  Pascal Gross Kukosa mkwaju wa penalty. Manchester City wakaendeleza ushindi wao mechi ishirini bila kupigwa baada ya Ruben Dias na John Stones kuipatia ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya Westham. Wana Nyundo hao walipata bao la kufutia machozi kupitia mshambuliaji wao Mikel Antonio.

Soko Directory is a Financial and Markets digital portal that tracks brands, listed firms on the NSE, SMEs and trend setters in the markets eco-system.Find us on Facebook: facebook.com/SokoDirectory and on Twitter: twitter.com/SokoDirectory

Trending Stories
Related Articles
Explore Soko Directory
Soko Directory Archives