Mabao mawili ya Pierre Emerick Aubameyang iliwezesha Arsenal kufuzu katika awamu ya kumi na sita kwenye michuano ya Europa baada kuibandua Benfica ya Ureno.
By Antonney Oduor
Mabao mawili ya Pierre Emerick Aubameyang iliwezesha Arsenal kufuzu katika awamu ya kumi na sita kwenye michuano ya Europa baada kuibandua Benfica ya Ureno.
Gunners walitoka nyuma na kuandikisha ushindi mkubwa baada ya Benfica kudhani kwamba watafuzu. Arsenal ilifungua ukurasa wa mabao baada ya nahodha wa Aubameyang kupata pasi murua kutoka kwa Bukayo Saka.
Dakika moja kabla ya mapumziko Benfica walijibu mapigo kupitia mkwaju wa adhabu na mchezji wao mahiri Diogo Goncalves. Kipindi cha pili makosa ya Dani Ceballos iliifanya kuwa nyuma tena baada ya Rafa Silva kufunga katika dakika ya sitini na moja.
Arsenal hawakukata matumaini kwani walikuwa na Imani kwamba watashinda. Beki wao Kieran Tierney alifunga bao la kusawazisha katika dakika ya sabini na tano. Arsenal walihitaji bao moja tu kufuzu na mkombozi wao Aubameyang alijitokeza wakati mashabiki wa Arsena walimhitaji sana na kufunga bao la ushindi.
Leicester ilipata adhabu ya kushangaza Sanaa baada ya kubanduliwa na Sparta Prague mabao mawili bila jawabu. Manchester united walitoka sare tasa na Real Sociedad ila walifuzu maana katika awamu ya kwanza waliadhibu timu hiyo kutoka ufaransa mabao manne kwa nunge. Mchezaji wa Sociedad aliwanyima mashabiki hao bao la kufutia machozi baada ya kukosa mkwaju wa Penalti.
Ajax ilifuzu baada ya kuibandua Lille ya Ufaransa, Molde ikatinga katika awamu ya kumi na sita bora baada ya kuitoa Hoffenheim, Napoli walititigwa na Granada ya uhispania hivo basi kukosa kupata tiketi ya kumi na sita bora. Villareal wa Unai Emery pia walikuwa miongoni wa wenye walifuzu baada ya kuibadua Salzburg ya Austria. Ac Milan, As Roma, Young Boys, Olympiacos, Dianamo Zagreb na Dynamo Kyiv wote wakapata tiketi ya kumi na sita bora.
Droo ya Europa itafanyika leo saa nane kule Urusi kubaini awamu nyengine itakuwa vipi na kutachezwa wapi.
Wikendi hii kutakuwa na mechi za Uingereza ambapo Chelsea wataialika mashetani wekundu ugani Stamford Bridge, kule King Power Leicester wwatacheza na washika bunduki wa Arsenal na vinara wa ligi Manchester city watakuwa Etihad kuikaribisha Westham, Liverpool watcheza na vibonde Sheffield United huku Spurs wakicheza na Burnley.