Borrusia Dortmund pia waliandikisha ushindi mwembamba huko ugenini baada kuichapa Sevilla mabao matatu kwa moja huko Uhispania.
By Antonney Oduor
Mabingwa wa Italia Juventus waligaragazwa mabao mawili kwa moja na klabu kutoka ureno ya Porto hapo jana usiku. Katika mechi iliyokuwa ya kusisimua, Fc Porto walifungua ukurasa wa mabao kupitia mshambuliaji wao Mehdi Taremi baada ya sekende arobaini na tano.
Waliongeza la pili kupitia mshambualiaji wao wa kati dakika moja baada kutoka mapumzikoni kipindi cha pili. Wana wa Juventus walijikakamua kufunga bao la kufutia machozi kupitia mshambulizi wao Federico Chiesa katika dakika za lala salama. Hii inaifanya Porto kuwa guu moja ndani katika raundi lakini itabidi wajikazee Kamba kwani haitakuwa rahisi kuibandua Juventus.
Borrusia Dortmund pia waliandikisha ushindi mwembamba huko ugenini baada kuichapa Sevilla mabao matatu kwa moja huko Uhispania. Erling Haaland alifunga mabao mawili kuiwezesha timu yake kuwa na nafasi nzuri ya kufuzu katika droo yar obo fainali.
Mechi hiyo ambayo ilichezwa bila mashabiki ilikua ya kusisumua sana. Sevilla walitangulia kufunga kupitia mchezaji wao mahiri Suso baadae Dortmund wakajibu mapigo kupitia kiungo wao Mahmoud Dahoud ndo baadae Halaand akafunga mawili. Luuk De Jong alijaribu kufufua matumaini ya Sevilla kutoka sare lakini muda ulikuwa umeyoyoma.
Kule Uingereza ni kwamba vinara wa ligi kuu Manchester City waliendeleza rekodi yao nzuri ya kushinda mechi Zaidi ya kumi na tano mfululizo. Jana katika uga wa Goodison Park wana wa Pep Guardiola walionyesha ubabe wao kwa kuifunga Everton mabao matatu kwa moja. Mabao ya City yalifungwa na Phil Foden, Ryard Mahrez na Benardo Silva kutamatisha ukurasa huo wa mabao.
Everton wakapata bao la kufutia angalau chozi lao kupitia mshambualiaji wao Richarliso. Ikumbukwe kwamba City wanaongoza jedwali na hamsini na sita, alama kumi Zaidi ya wapinzani wao. Hii inaifanya City kuwa nafasi nzuri ya kulibeba taji hilo ya Uingereza kwa mara ya pili chini ya Mkufunzi wao Pep Guardiola.
Barani ya ulaya mashindano ya Europa yatang’oa nanga leo usiku huku Arsenal inaenda kucheza na Benfica kule uitaliano uwanja wa Stadio Olimpico, Roma. Manchester United watacheza na Real Sociedad huko Turin huku Napoli wakicheza na Granada. Baadhi ya mechi hizo hazitacgezwa kwa uwanja tulizozitarajia kulingana na sheria kali za korona.
About Author
A freelance Journalist Who has much interest in sports and trends. He says it as it is and brings out the bitter truth and the thrill in the game.