Mechi iliyoshuhidia ubabe sana maana kila pande ilidhihirisha ya kwamba walikuwa wamejiandaa sana kujitupa uwanjani lakini mwisho wa siku timu bora iliibuka na ushindi.
By Antonney Oduor
Vinara wa Ligi Kuu Uingereza Manchester City waliibuka na ushindi mwembamba dhidi ya washika bunduki wa Arsenal hapo jana.
Mechi iliyoshuhidia ubabe sana maana kila pande ilidhihirisha ya kwamba walikuwa wamejiandaa sana kujitupa uwanjani lakini mwisho wa siku timu bora iliibuka na ushindi.
Wana wa Pep waliipata bao lao la kipekee katika kipindi cha kwanza dakika ya pili kupitia winga wao mahiri Raheem Sterling. Arsenal walijitahidi kukomboa lakini juhudi zao ziligonga mwamba. Man City wanaongoza jedwali hilo na alama kumi Zaidi ya mahasimu wao wa jadi Manchester United wanaoshikilia nafasi ya pili.
Manchester United nao pia waliandikisha ushinidi mzuri wa mabao matatu kwa moja dhidi ya wapinzani wao Newcastle. Marcus Rashford alifungua ukurasa wa mabao katika dakika ya thelathini huku Saint Maximin akisawazishia Newcastle dakika sita baadae.
Katika kipindi cha pili Daniel james alifunga la pili na kuifanya United kuwa na ushindi wao huku Bruno Fernandes akifunga la tatu la tatu kupitia mkwaju wa penalty. Mashetani hao wekundu wanashikilia nafasi ya pili na alama aubaini na tisa.
Kwengine ni kwamba Leicster walichapa Aston Villa Ugenini mabao mawili kwa moja. Vijana wa Mourinho Tottenham Hotspurs walicharazwa na Westham mabao mawili kwa moja. Sheffield walizidi kutupa alama na kubakia mwisho kwenye jedwali baada ya kufungwa na Fulham.
Everton walipata ushindi wao mkubwa dhidi ya Liverpool ya mabao mawili kwa nunge. Hii ilikuwa mara ya kwanza Liverpool kupoteza nyumbani wakicheza na Everton mahasimu wao wa jadi katika karne hii. Wana wa Klop wameandikisha historia mbaya zadia tangu mwaka wa 1923 kupoteza nyumbani mara tatu mfululizo. Chelsea nao walitoka sare ya bao moja na Southampton.
About Author
A freelance Journalist Who has much interest in sports and trends. He says it as it is and brings out the bitter truth and the thrill in the game.