Skip to content
Entertainment

Pep Aendeleza Rekodi Ya Kutofungwa, Real Wapata Ushindi

BY Soko Directory Team · February 25, 2021 10:02 am

KEY POINTS

City wanaendeleza msururu wao wa ushindi ya Zaidi ya mechi kumi na nane bila kufungwa. Hii ni baadhi ya rekodi chache ambazo haziwaji fungwa na team yeyote chini ya mkufunzi Pep Guardiola.

By Anthonney Oduor

Vinara wa Ligi Kuu Ya Uingereza Manchester City waliendeleza rekodi yao nzuri ya kuchovya asali ya ushindi pale ambapo walipata ushindi mwengine dhidi ya wapinzani wao Borussia Monchengladbach mabao wawili kwa nunge walipokuwa wanacheza ugenini.

City wanaendeleza msururu wao wa ushindi ya Zaidi ya mechi kumi na nane bila kufungwa. Hii ni baadhi ya rekodi chache ambazo haziwaji fungwa na team yeyote chini ya mkufunzi Pep Guardiola. Mwisho alifanya ilikuwa mechi kumi na tatu bila kufungwa akiwa mkufunzi wa Bayern Munch. Mabao ya vigogo hao kutoka uingereza yalifungwa na Bernado Silva na Gabriel Jesus kuikata matumaini ya wajerumani wale kutofuzu katika awamu nyengine katika michuano haya. Vijana hao wa Pep wanapigiwa upato sana kulibeba taji la Uingereza n ahata barani ulaya.

Licha ya kadi nyekundu katika dakika kumi na saba kwa wana wa Atalanta kwa mechazaji wao Remo Freuler, waitaliano hao walikaza Kamba angalau wapate sare lakini mfaransa Ferland Mendy alidhihirisha ubabe wake mbele ya kocha wake Zinadine Zidane ambaye ni mfaransa mwenzake, ili kuipatia klabu yake ya Real Madrid ushindi mwembamba ugani Gewiss. Real ambayo inakosa huduma za wachezaji wao muhimu bado wana mlima wa kuupanda kwani mechi za marudiano kutakuwa na hamaki kubwa sana viwanjani. Ushindi huo bado haijaptia wana Los Blancoos tiketi ya kufuzu.

Kule Europa ni kwamba washika bunduki wa Arsenal watashuka dimbani kumenyana na Benfica ili kupata alama muhimu ya kuiwezesha kufuzu katika kumi na sita bora katika michuano haya. Mechi ya leo inakisiwa kuwa fainali kwa wana hao wa Arteta ambae wachezaji wake muhimu kama Thomas Partey na Kieran Tierney.

Kwengineko ni Kwamba Ajax wataikaribisha Lille, Granada kualikwa na Napoli, As Roma kuialika Brag na Manchester United kuialika Real Sociedad.

Usikose kushuhudia mechi hizi ukitaka kuwa na usiku mwanana unapopanga mbavu zako kuelekea dunia ya wenyewe.

Soko Directory is a Financial and Markets digital portal that tracks brands, listed firms on the NSE, SMEs and trend setters in the markets eco-system.Find us on Facebook: facebook.com/SokoDirectory and on Twitter: twitter.com/SokoDirectory

Trending Stories
Related Articles
Explore Soko Directory
Soko Directory Archives