Skip to content
Entertainment

Palace Wafisha Matumaini Ya United Kukaribia City

BY Soko Directory Team · March 4, 2021 08:03 am

KEY POINTS

Mashetani wekundu walitoka sare ya bao tasa na Crystal Palace ugani Selhurst jana katika mechi iliyokuwa haina utamu sana kama ilivyo tarajiwa.

By Antonney Oduor

Mashetani wekundu walitoka sare ya bao tasa na Crystal Palace ugani Selhurst jana katika mechi iliyokuwa haina utamu sana kama ilivyo tarajiwa.

Matumaini ya United kuikaribia City katika kuwania taji la ligi kuu msimu huu inazidi kudidimia kila uchao kwani wanazidi kupoteza alama huku city inazidi kupenya kwani sai wako mbele na alama kumi na nne.

Mkufunzi Mkuu wa United Ole Gunnar alioonyesha kugadhabishwa na matokeo hayo jamaa ambazo hakutarajia. United inazidi kushika nafasi ya pili na alama hamsini na moja. Tangu Januari ishirini na nne Mashetani hao wekundu wamepoteza alama kumi na tano.

Vibonde Sheffield United walijizatiti mbele ya wapinzani Aston Villa baada ya kutoka na ushindi mwembamba dhidi yao hapo nyumbani Bramall Lane. Bao la kipekee lilifungwa na  David McGoldrick katika dakika ya thelathini baada ya kupokea pasi ya kiufundi sana kupitia George Baldock.

Aston Villa walijaribu kuweka mambo sawa lakini juhudi zao ziligongamwamba na kuambulia patupu. Baaadae Phil Jagielka akachezwa ndivyo sivyo na baadae kuonyesha kadi nyekundu katika dakika ya hamsini na saba. Sheffield walijikakamua na hatimae kutoka na alama tatu muhimu.

Mabingwa wa mwaka 2015/2016 Leicester walizidi kupoteza alama baada ya kuzuia na kutoka sare ya moja dhidi ya wapinzani wao Burnley pale Turf Moor. Burnley walifungua ukurasa wa mabao baada ya Matej Vydra kupachika katika dakika ya nne huko mwanzoni mwa mchezo baadae Kelechi Iheanaacho alijibu mapigo na kufanya mambo yawe sare kabisa na hatimae mchezo ukaishi hivo. Leicester bado wanashikilia nafasi ya pili wakiwa na alama hamsini.

Leo Liverpool itaialika Chelsea ugani Anfield kwa mechi inayongojewa kwa ham una hamumu. Ikumbukwe kwamba Chelsea hawajapoteza mechi yeyote chini ya mkufunzi wao mpya Thomas Tuchel. Liverpool katika mechi tatu zilizopita wamekuwa na rekodi ya kufungwa sana isipokuwa mechi yao dhidi ya Sheffield. West Brom wataialika Everton pale Hawthorns huku Fulham watapeperusha bendera yao tena wakitumainia kupata ushindi dhidi ya Tottenham Hotspurs.

Kwengineko ni kwamba Barcelona imefuzu katika fainali ya Copa Del Rey baada ya kuibandua Sevilla mabao matatu katika mechi iliyokuwa na msisimko sana. Wana Catalunya hao walipata ushindi katika awamu ya pili ya mchezo huo baada ya kufungwa mabao mawili kwa nunge katika awamu ya kwanza. Mabao hayo yalifungwa na Ousmane Dembele, Gerard Pique na Martin Braithwaite kufunga katika dakika ya ziada.

READ: Mashetani Wekundu Watisha, Huku Arsenal Ikitoka Sare

Soko Directory is a Financial and Markets digital portal that tracks brands, listed firms on the NSE, SMEs and trend setters in the markets eco-system.Find us on Facebook: facebook.com/SokoDirectory and on Twitter: twitter.com/SokoDirectory

Trending Stories
Related Articles
Explore Soko Directory
Soko Directory Archives