Skip to content
Entertainment

Tuchel Hakamatiki, Inter Milan Wazidi Kupaa

BY Soko Directory Team · March 9, 2021 11:03 am

KEY POINTS

Thomas Tuchel alizidi kuendeleza rekodi yake nzuri baada ya kutofungwa tena katika ligi kuu uingereza. Jana katika uga wa Stamford Bridge Chelsea waliandikisha ushindi mwengine wa mabao mawili bila jawabu dhidi ya wapinzani wao Everton.

Thomas Tuchel alizidi kuendeleza rekodi yake nzuri baada ya kutofungwa tena katika ligi kuu uingereza. Jana katika uga wa Stamford Bridge Chelsea waliandikisha ushindi mwengine wa mabao mawili bila jawabu dhidi ya wapinzani wao Everton.

Mabao hayo yalifungwa na Muitaliano Jorginho kupitia mkwaju wa penalty na lengine walizawadiwa na Everton baada ya Ben  Godfrey kujifunga katika lango lake.Khai Havertz aifunga bao murwa ila sheria za Var ilikataa bao hilo baada ya kusemekana alikuwa ameunawa mpira huo. Hii inaifanya Chelsea kukaa nafasi ya nne huku Everton wakisalia nafasi ya sita.

Westham nao waliandikisha ushindi mwengine baada kuichapa leeds mabao mawili kwa nunge ugani London. Mabao hayo yalifungwa Jesse Lingard na  Craig Dawson. Mabao haya yalikuja baada ya mabao mawili ya leeds kukataliwa na Var. Hii inaiweka Westham katika nafasi ya tano.

Kule uitaliano Inter Milan waliendeleza kushika usukani katika ligi ya Serie A baada ya kuichapa Atalanta bao moja kwa sufuri. Bao hilo la kipekee lilifungwa na Milan Skriniar katika dakika ya hamsini nan ne. hii inaifanya Inter kua katika nafasi ya kwanza mbele ya Ac Milan na Juventus.

Kule barani ulaya pia leo kutakuwa na kiputepute dimbani baada kuwa na awamu ya pili ya mechi hizo. Borussia Dortmund itacheza na Sevilla ugani Signal Iduna Park leo huku Juventus ikiwa wenyeji wa Fc Porto pale Turin. Mechi hizo zitakuwa za mwisho katika ya timu ili kufuzu katika awamu yar obo fainali.

Soko Directory is a Financial and Markets digital portal that tracks brands, listed firms on the NSE, SMEs and trend setters in the markets eco-system.Find us on Facebook: facebook.com/SokoDirectory and on Twitter: twitter.com/SokoDirectory

Trending Stories
Related Articles
Explore Soko Directory
Soko Directory Archives