Skip to content
Entertainment

Mabingwa Wa Ufaransa Wafika Nusu Fainali, Chelsea Wafuzu Pia

BY Soko Directory Team · April 14, 2021 10:04 am

KEY POINTS

PSG ya Ufaransa imejikatia Tiketi ya kucheza katika awamu ya nusu fainali ya Ligi Ya Mabingwa barani ulaya. Hii ni baada ya kuibandua mabingwa watetezi Bayern Munich katika awamu Ya Robo fainali.

PSG ya Ufaransa imejikatia Tiketi ya kucheza katika awamu ya nusu fainali ya Ligi Ya Mabingwa barani ulaya. Hii ni baada ya kuibandua mabingwa watetezi Bayern Munich katika awamu Ya Robo fainali.

Jana Usiku Vinara hao wa Ujerumani walitoka na ushindi wa bao Moja bila jawabu lakini katika Mkondo wa kwanza walichapwa mabao matatu kwa mawili, hivyo basi sheria za Ulaya hazikuruhusu Bayern Kufuzu Kwani walikuwa wamefungwa mabao za nyumbani tatu. Sheria inayoitwa “away goal rule”. Bao hilo la kipekee lililofungwa na Maxim Choupo-Moting.

Chelsea pia hawakuachwa nyuma katika kuwania awamu za nusu fainali baada pia hao Kufuzu katika shehena ya nusu fainali licha ya kufungwa bao Moja na wareno kutoka Porto. Porto waliibuka na ushindi wa moja bila jawabu ila vijana wa Tuchel walikuwa na Mabao mawili zaidi.

Hivyo basi Chelsea itaenda kupatana na mshindi kati ya Liverpool na Real Madrid huku PSG watacheza na Mshindi wa Manchester City na Borrusia Dortmund.

Leo katika michuano  ya Ulaya Manchester City Wataniua Kufuzu katika awamu ya Nusu Fainali baada kuwa kifua mbele na Mabao mawili. Huku Real Madrid wanataka tu sare dhidi ya Liverpool ndo wafuzu. Itakuwa kiputepute kikubwa. Kwani wanasema fahali wawili wanapopigana Nyasi ndizo huumia. usikose kushuhudia uhondo huu ambao ni zaidi ya Iftar ama daku.

Soko Directory is a Financial and Markets digital portal that tracks brands, listed firms on the NSE, SMEs and trend setters in the markets eco-system.Find us on Facebook: facebook.com/SokoDirectory and on Twitter: twitter.com/SokoDirectory

Trending Stories
Related Articles
Explore Soko Directory
Soko Directory Archives