Skip to content
Entertainment

Mabingwa Watetezi Wapigwa, Chelsea Kujipa Njia Rahisi

BY David Indeje · April 8, 2021 10:04 am

KEY POINTS

Bayern Munich Walipata kuona usiku mrefu ndani ya Allianz Arena baada kupokea kichapo cha tatu mbili kutoka kwa mahasimu wao wa jadi Ulaya Paris Saint Germain.

Na Antonney Oduor

Bayern Munich walipata kuona usiku mrefu ndani ya Allianz Arena baada kupokea kichapo cha tatu mbili kutoka kwa mahasimu wao wa jadi Ulaya Paris Saint Germain.

Mabao mawili ya Kylian Mbappe yalitosha kuipa ushindi wafaransa hao na kuigaragaza Bayern Munich. Mabao ya Wajerumani hao Yalifungwa na Choupo Mouting na Thomas Muller na bao lengine la PSG lilifungwa na Marquinhos.

Matokeo haya huenda Yakawa magumu kwa Bayern Munich Kwani tayari PSG Wana mabao matatu ya ugenini. Inasemekana PSG ilikuja kulipiza kisasi ya Fainali zilizopita baada ya kuchapwa na Bayern Munich katika fainali za Barani ulaya.

Chelsea walitia guu Moja katika awamu ya nusu fainali baada ya kuitibua Fc Porto Ya Ureno mabao mawili kwa nunge. Mabao hayo Yalifungwa na Mason Mount na Ben Chilwell na kuhaikishia Chelsea wanakuwa na nafasi nzuri ya kucheza katika awamu nyengine.

Inakisiwa Kwamba hata Wana Blues wakipata sare ya kutofungana basi watakuwa washafuzu katika nusu fainali. Matokeo haya yanakuja baada ya Chelsea kuwa matokeo mabaya kwa ligi kuu Uingereza.

Kule Uitaliano kwenye Ligi ya Serie A Juventus waliwakandamiza wapinzani wao Napoli kwa mabao mawili kwa Moja. Mshambuliaji wao Cristiano Ronaldo alifungua ukurasa wa mabao huku Paulo Dybala kuongeza la pili.

Napoli walipata bao la kufutia machozi kupitia mshambuliaji wao Insigne. Hii inaifanya Juventus kushikilia nafasi ya Tatu kwenye jedwali huku Inter Milan ilizidi kushika usukani.

Leo kutakuwa na mechi za Ligi ya Europa awamu ya kwanza ya robo fainali. Arsenal wataialika Slavia Praha katika uga wao wa Emirata, Granada wataalika mabingwa wa Europa mwaka wa 2017 Manchester United. Huku Ajax wakiminyana na Roma na hatimaye Dianamo Zagreb Kupambana na Villarreal ya Unai Emery.

Usikose kushuhudia mapambano haya Kwani ina ladha zaidi ya Asali.

David Indeje is a writer and editor, with interests on how technology is changing journalism, government, Health, and Gender Development stories are his passion. Follow on Twitter @David_IndejeDavid can be reached on: (020) 528 0222 / Email: info@sokodirectory.com

Trending Stories
Related Articles
Explore Soko Directory
Soko Directory Archives