Skip to content
Entertainment

Mbuzi Kala Mkeka, Kivumbi Chativuka Ugani

BY Soko Directory Team · April 15, 2021 08:04 am

KEY POINTS

Jude Bellingham Alianza kutingisha ulinzi wa City katika dakika kumi na tano alifunga bao murua lakini ilikuwa ni kama kuenda kwenye mzinga wa nyuki kutingiza ilikuwa ni dhihaka kwa Wana wa Citizens.

Na Antonney Oduor

Hayawi, hayawi, yasiyokuwa Yakawa. Wanasema Mbiu ya Mgambo ikilia basi Huwa kuna jambo. Nusura mende kuangusha kabati katika uga wa Induna Park kule Ujerumani pale ambapo Borrusia Dortmund walipotaka kufuzu katika awamu ya nusu fainali.

Jude Bellingham Alianza kutingisha ulinzi wa City katika dakika kumi na tano alifunga bao murua lakini ilikuwa ni kama kuenda kwenye mzinga wa nyuki kutingiza ilikuwa ni dhihaka kwa Wana wa Citizens.

Katika kipindi cha pili Manchester City walijipanga na kupata mkwaju wa penalti ambapo Riyard Mahrez alitia kimyani katika dakika ya hamsini na tisa na Kabla ya kinda kutoka Uingereza Phil Phoden kufunga bao la ushindi na kubakikisha Kwamba Dortmund wanaenda nyumbani na hao wanafuzu katika awamu ya nusu fainali. Vinara hao wa Uingereza wanapigiwa sana upato wa kuibeba taji hilo la Barani Ulaya Tena sana.

Sare katika uga wa Anfield ilitosha kuipeleka mabingwa mara kumi na tatu katika nusu fainali.

Real Madrid ambao kule Uhispania walifunga Liverpool mabao matatu kwa.moja walihitaji tu sare ndiposa waendeleze. Halaiki ya watu ilingoja miujiza ya Anfield lakini mizimu yao haikusimama tisti na bahati haikuwa katika upande wao kabisa. Real Madrid wakaamua kucheza mechi ya sare.

Hivyo basi siku kumi na tatu kwanzia leo ndio tutashuhudia Nusu Fainali katika.Ya Mabingwa wa Ufaransa Paris Saint German na Vinara wa Uingereza Manchester City. Upandee mwengine ni Kwamba Real Madrid watacheza na Chelsea. Mechi hizi ndizo zitakazo simamisha Dunia katika Juma zijazo.

Na kule Europa Washika bunduki Wa Arsenal wanatafuta ushindi wa aina yeyote ili Kufuzu dhidi ya Slavia Prague kule Urusi. Manchester United watacheza na Granada, Villarreal na Dinamo Zagreb huku Roma wakipambana na Ajax. Usikose kutazama mechi hizi usiku wa leo mwendo wa Saa nne kamili.

Soko Directory is a Financial and Markets digital portal that tracks brands, listed firms on the NSE, SMEs and trend setters in the markets eco-system.Find us on Facebook: facebook.com/SokoDirectory and on Twitter: twitter.com/SokoDirectory

Trending Stories
Related Articles
Explore Soko Directory
Soko Directory Archives