Skip to content
Entertainment

Kiburi Cha Mourinho Chalipuliwa Na Washika Bunduki.

BY Soko Directory Team · March 15, 2021 10:03 am

KEY POINTS

Hayawi huwa yasiyokuwa yakawa, jana katika uga wa Emirata Arsenal walinyamanzisha kiburi na mabezo  ya Jose Mourinho baada ya kuwapa kichapo cha mbwa kutabasaki msikitini baada ya kucharazwa mabao mawili kwa moja.

By Antonney Oduor

Hayawi huwa yasiyokuwa yakawa, jana katika uga wa Emirata Arsenal walinyamanzisha kiburi na mabezo  ya Jose Mourinho baada ya kuwapa kichapo cha mbwa kutabasaki msikitini baada ya kucharazwa mabao mawili kwa moja. Erick lamella alifungua ukurasa wa karamu ya mabao baada kutangulia kuiweka spurs mbele baada ya dakika thelathini na sita.

Martin Odergaard alijibu mapigo dakika mbili kabla ya mapumziko. Alexandre Lacazette aliiweka Arsenal kifua mbele baada kufunga mkwaju wa penalty dakika sitini na nane. Haikuwa siku nzuri kwa Erick lamele ambae aliingia dakika kumpumzisha Son ambaye aliandamwa na majeruhi, alionyesha kadi nyekundu baada kumchezea ndivyo sivyo Kieran Tierney katika dakika na sabini na tano. Mourinho aligadhabishwa san ana wachezaji huku Mikel Arteta akiwapongeza kila mchezaji wake baada ya kipenga cha mwisho.

Bao la kujifunga la Craig Dawson ilitosha kuwapa mashetani wekundu wa Manchester alama tatu muhimu baada bao hilo la kipekee. Westham walijizatiti lakini juhudi zao ziligonga mwamba na hatimaye mechi hiyo kuisha bao moja kwa nunge. Leicester iliwaadhibu Sheffield United mabao matano kwa nunge ugani king Power.

Mabao hayo yalifungwa na Kelechi Iheanacho mabaye alifunga matatu, huku Ayoze Perez na bao la kujifunga la Ampadu ilitosha kuipa wana hao wa Foxes ushindi. Brighton pia ikaichapa Southampton mabao mawili kwa moja.

Chelsea walitoka sare ya bila kufunga na Leeds, Vinara Manchester City wakaichapa Fulham mabao matatu kwa nunge na hatimaye Burnley kuandikisha matokeo ya kustaajabisha sana baada kuichapa Everton mabao mawili kwa moja.

Kule uitaliano ni kwamba Cristaino Ronaldo alipachika nyavuni mabao matatu dhidhi ya wapinzani wao Cagliari. Juventus iliandika ushindi huo baada ya kubaduliwa katika ligi ya mabingwa ulaya na kupata alama muhimu. Napoli iliichapa AC Milan bao moja kwa sufuri, Parma ikafuta matumaini ya Roma kupata alama tatu baada ya kuinyuka mabao mawili bila jawabu. Huku Inter Milan wakiendeleza ushindi wao baada ya kuichapa Torino mabao mawili kwa moja.

Soko Directory is a Financial and Markets digital portal that tracks brands, listed firms on the NSE, SMEs and trend setters in the markets eco-system.Find us on Facebook: facebook.com/SokoDirectory and on Twitter: twitter.com/SokoDirectory

Trending Stories
Related Articles
Explore Soko Directory
Soko Directory Archives