Pep Guardiola anazidi kuvunja rekodi ya Arsenal iliyowekwwa mwaka 1998/1999 ya kushinda mechi ishirini mfululizo.
By Antonney Oduor
Pep Guardiola anazidi kuvunja rekodi ya Arsenal iliyowekwwa mwaka 1998/1999 ya kushinda mechi ishirini mfululizo. Jana katika uga wa Etihad Manchester ilizidi kupaa kileleni baada ya kuipa adabu Wolves hapo usiku kwa mabao manne kwa moja.
Magoli hayo yalifungwa bao la kujifunga kupitia mchezaji wa Wolves Leander Dendoncker, ila waliporudi kipindi cha pili wana Mbweha hao walijibu mapigo na kusawazisha mambo kupitia Conor Coady. Baada ya wapinzani hao wa City kufanya mambo yawe sare kumbe walichokoza nyuki mzingani.
Pep alibadilisha mtindo wa kucheza kuifanya safu yake ya ushambuliaji kuwa na makali Zaidi kwa Gabriel Jesus alifunga mawili huku Ryard Mahrez kufunga moja kuifanya City kuibuka na ushindi wa mabao manne. Ushindi huu inaieka wana wa Pep kileleni na alama kumi na tano mbele.
Mabingwa mara sab akule Italia, Juventus walifufua matumaini yako ya kutwaa taji la Serie A baada ya kuigaragaza klabu ya Spezia mabao matatu kwa nunge mchezo uliochezwa Allianz huko Turin. Mabao hayo yalifungwa kipindi cha pili kupitia wachezaji wao Alvaro Morata, Federico Chiesa, na Cristiano Ronaldo. Ushindi huu inaifanya Juventus kushikilia nafasi ya tatu nyuma ya Ac Milan na Inter Milan. Ambao wako mbele yao na alama saba.
Leo katika ligii kuu uingereza ni kwamba Burnley wataialika Leicester pale Turf Moor, huku Aston Villa wakienda ugenini Bramall Lane kupambana vikali na Sheffield United ambao wanashikilia nafasi ya mwisho jedwalini. Kule ugani Selhurst Crystal Place watawakaribisha mashetani wekundu wa Manchester hapo baadae ili kubaini mbivu na mbichi. Mechi zote zitachezwa saa tano usiku itakuwa awamu ya ishirini na tisa ya ligii kuu.
READ: Pep Aendeleza Rekodi Ya Kutofungwa, Real Wapata Ushindi