Tottenham walitoka sare ya mabao mawili kwa mawili na Newcastle huku Aston Villa iliigaragaza Fulham mabao matatu kwa Moja.
Na Antonney Oduor
Rekodi nzuri ya Mjerumani Thomas Tuchel ya kutofungwa katika mechi zake za kwanza zilitumbukia Nyongo baada ya kupewa kichapo cha mbwa aliyetabasaki msikitini.
Chelsea walifunzwa adabu kama venye Maulan aliwafunza Sodoma na Gommorrah baada ya kuchapwa mabao matano kwa mawili na timu ambayo inashikilia nafasi ya kumi na tisa katika jedwali na Westbromwich Albion.
Chelsea walianza kunyeshewa karamu ya mabao baada mlinzi wao mkongwe Thiago Silva kuonyeshwa kadi ya njano ya pili na hatimaye kuwa nyekundu.
Christian Pulisic alifungua ukurasa wa mabao upande wa chelsea kumbe walichokoza nyuki na Matheus Pereira kutiwa mawili kabla kipindi cha kwanza.
Diagne na Robinson kuongeza mawili na kufanya idadi ya mabao kuwa tano. Mason Mount alifunga LA kutoa machozi kwa upande wa chelsea na kufanya mabao Kuzidi unga. Arsenal nao pia wakachapwa na Liverpool ugani kwao Emirates. Salah na Jota ambaye alitia mawili. Na kufanya idadi kuwa tatu kwa mtungi.
Mashetani wekundu nao walitoka nyuma kuilima Brighton mabao mawili kwa Moja. Mchezaji wa kitambo Wa United Danny Welbeck alifungua ukurasa wa mabao na kuiweka Brighton kifua mbele katika dakika ya kumi na Nne baada Ya Rashford kukomboa na kuweka mambo kuwa Sawa.
Bao la ushindi lilifungwa na Mason GreenWood dakika za salama. Vinara wa Ligi Manchester City waliinyuka Leicester mabao mawili kwa nunge baada Ya Benjamin Mendy na Gabriel Jesus kufunga mabao hayo na kuiweka City kifua mbele katika jedwali.
Tottenham walitoka sare ya mabao mawili kwa mawili na Newcastle huku Aston Villa iliigaragaza Fulham mabao matatu kwa Moja.
Kule Uhispania ni Kwamba ndoto za Athletico Madrid kutwaa taji la La Liga linazisi kudidimia baada ya jana kuchapwa na Sevilla bao Moja kwa nunge.
Ufaransa ni Kwamba Lille wanaongoza jedwali baada ya kuishanganza Dunia kwa kuichapa PSG bao Moja kwa sufuri.
Kule Ujerumani pia Bayern walitoka na ushindi mwembamba dhidi ya Leizpig ya bao Moja kwa nunge.
Usisahau Kwamba wiki hii kutakuwa na mechi kubwa za klabu bingwa Ulaya na Europa