Mabingwa wa Ulaya kwa mara ya kumi na tatu Real Madrid Hapo Jana katika uga wa Alfredo De Stefano waliwacharaza mabingwa mara sita Liverpool mabao matatu kwa Moja.
Na Antonney Oduor
Mabingwa wa Ulaya kwa mara ya kumi na tatu Real Madrid Hapo Jana katika uga wa Alfredo De Stefano waliwacharaza mabingwa mara sita Liverpool mabao matatu kwa moja.
Wana Los Blancos walifungua ukurasa wa mabao kupitia kinda wao Vinicius Junior baada ya kupokea pasi murwa kutoka kwa Mjerumani Toni Kroos katika dakika ya ishirini na sita.
Wana Reds maji iliwazidi unga Kwani kabla ya dakika chache ndo waende mapumzikoni walifungwa lengine kupitia Mchezaji Marco Asensio.
Klop alikuwa amepaniki baada ya kumtoa Baby Keita katika dakika za arubaine. Kipindi cha pili kurudi Liverpool walijikakamua kupata bao la kufutia machozi kupitia Mchezaji wa mshambuliaji Mohamed Salah na kufanya mambo kuwa mawili kwa Moja.
Katika dakika ya sitini na tano Vinicius Junior alipokea Tena pasi kutoka kwa Mkrotia Luka Modric na kuchapa msumari wa mwisho kwenye Jeneza alipofunga bao la tatu na la ushindi. Hivyo Basi Liverpool Wana kibarua kigumu watakapocheza kule Anfield wiki ijayo. Je kutakuwa na miujiza ya Anfield ama tusuburie dakika tisini za mchezo.
Manchester City wametia guu Moja katika awamu ya Robo fainali baada ya kuwagaragaza Borrusia Dortmund mabao mawili kwa moja kule Etihad, Manchester. Nahodha wa Jana Kevin De Bruyne alifungua ukurasa mabao katika dakika ya kumi na saba kipindi cha kwanza na kuiweka City mbele. Dortmund walinyimwa bao la Jude Bellingham katika dakika ya thelathini baada ya mwamuzi Mkuu kuamua kuwa alikuwa amecheza ndivyo sivyo. Katika dakika za lala salama Marco Reus alifunga bao la kufutia machozi na kufanya mambo kuwa Sawa lakini katika dakika za ziada Phil Foden alihakikisha Kwamba city wanatoka na ushindi.
Leo kutakuwa na pambano katika Ya PSG na Bayern Munich. PSG watakosa huduma Za Mchezaji wao Marco Verrati ambae aliwekwa karantini baada ya kupatikana na virusi vya Covid-19, huku Bayern Munich watakosa huduma Za Mshambuliaji wao matata Roberto Lewandowski ambae anauguza jeraha la goti, Serge Gnabry ambae ana virusi Vya Covid. Mechi Hiyo itakuwa kumbukumbuku ya Fainali ambazo zilichezwa mwaka uliopita.
Chelsea waatalikwa kucheza Ureno na FC Porto. Mechi Hiyo ambae kila upande haina tatizo la majeraha sana lakini kuna baadhi ya wachezaji wa Chelsea ambao wamerudi. Ikiwa ni Ngolo Kante, Tammy Abraham na Thiago Silva. Chelsea watarudi uwwanjani baada ya wikendi iliyopita kuadhibiwa mabao matano na Westbrom.
Usikose kutazama mechi hizi Kwani itakuwa zaidi ya uhondo.