Man U Watoka Nyuma Na Kuwatandika Tottenham

By Soko Directory Team / Published April 12, 2021 | 11:30 am
KEY POINTS

Manchester United walitoka nyuma kuibuka na ushindi wa mabao mawili kwa Moja dhidi ya Wapinzani wao Tottenham Hotspurs kutoka london inayofunzwa na Mkufunzi Mahiri Jose Mourinho.
Na Antonney Oduor

Manchester United walitoka nyuma kuibuka na ushindi wa mabao mawili kwa Moja dhidi ya Wapinzani wao Tottenham Hotspurs kutoka london inayofunzwa na Mkufunzi Mahiri Jose Mourinho.

Spurs walifungua ukurasa wa mabao kupitia Mkorea Son baada ya Bao la United kukataliwa pale ambapo Son alichezewa ndivyo sivyo. Kipindi cha pili kilianza na vishindo sanaa Kwani Mashetani wekundu walijawa mori kana kwamba walikuwa wamechanjwa chale.

Fred Rodriguez raia wa kibrazili alifunga bao lake la kwanza baada ya miaka mitatu, Edison Cavani alifunga la pili baada ya kupokea pasi murua kutoka kwa kinda Mason GreenWood aliyeingia katika nafasi ya Marcus Rashford katika dakika za lala salama.

Paul Pogba alikuwa katika ubora wake kwenye mechi Hiyo baada ya kutoa pasi ambapo Mason GreenWood alitia msumari wa Mwisho katika sanduku la Vijana wa Mourinho. Hii inaifanya United kushikilia nafasi ya Pili na alama sitini na tatu.

Alexandre Lacazette alikuwa Mchezaji wa Kumi wa katika orodha ya Arsenal kufikisha mabao hamsini katika mechi za Ligi Kuu Uingereza. Jana katika uga wa Bramal Lane washika bunduki wa Arsenal waliibuka na ushindi wa tatu bila ambao unawapeleka hadi Nafasi ya tisa katika jedwali.

Nahodha wao wa siku Lacazette alitia mabao mawili huku kinda wao wa kibrazili Gabriel Martineli kufunga Moja. Lacazette siku Ya Alhamisi alikashifiwa mno baada ya kukosa nafasi ya wazi walipokuwa wanacheza na Slavia Prague. Arsenal wanakusudiwa kucheza mechi ya na Prague ya marudiano.

Manchester City walifungwa na wachezaji kumi wa leeds mabao mawili kwa Moja. Westham wakaichapa Leicester City mabao matatu kwa mawili, Chelsea wakaigaragaza Crystal Palace mabao manne kwa Moja. Newcastle wakaichapa Wolves mabao mawili kwa Moja.

Kule Uhispania ni Kwamba miamba wa Catalunya Barcelona walicharazwa mabao mawili kwa Moja dhidi ya wapinzani wao Real Madrid. Kareem Benzema alifungua ukurasa wa mabao baada ya Toni Kroos kufunga la pili. Barcelona walipata bao la kufutia machozi kupitia Mchezaji wao Mingueza.

Athletico Madrid walitoka sare na Real Betis hivyo nasi kufanya nafasi yao ya kuongoza jedwali kuwa mashakani mno. Kwani wanaongoza jedwali hilo na alama Moja mbele.

Endelea kupata uhondo wa spoti Kwani wiki hii kutakuwa na sherehe ya Ndovu kumfanya mwanawe kitoweo.

About Soko Directory Team

Soko Directory is a Financial and Markets digital portal that tracks brands, listed firms on the NSE, SMEs and trend setters in the markets eco-system.Find us on Facebook: facebook.com/SokoDirectory and on Twitter: twitter.com/SokoDirectory

View other posts by Soko Directory Team


More Articles From This Author


Trending Stories


Other Related Articles


SOKO DIRECTORY & FINANCIAL GUIDEARCHIVES

2021
 • January 2021 (182)
 • February 2021 (227)
 • March 2021 (325)
 • April 2021 (261)
 • May 2021 (104)
 • 2020
 • January 2020 (272)
 • February 2020 (310)
 • March 2020 (390)
 • April 2020 (321)
 • May 2020 (335)
 • June 2020 (327)
 • July 2020 (334)
 • August 2020 (276)
 • September 2020 (214)
 • October 2020 (233)
 • November 2020 (242)
 • December 2020 (187)
 • 2019
 • January 2019 (253)
 • February 2019 (216)
 • March 2019 (285)
 • April 2019 (254)
 • May 2019 (272)
 • June 2019 (251)
 • July 2019 (338)
 • August 2019 (293)
 • September 2019 (306)
 • October 2019 (313)
 • November 2019 (362)
 • December 2019 (319)
 • 2018
 • January 2018 (291)
 • February 2018 (213)
 • March 2018 (278)
 • April 2018 (225)
 • May 2018 (237)
 • June 2018 (178)
 • July 2018 (256)
 • August 2018 (249)
 • September 2018 (256)
 • October 2018 (287)
 • November 2018 (284)
 • December 2018 (186)
 • 2017
 • January 2017 (183)
 • February 2017 (194)
 • March 2017 (207)
 • April 2017 (104)
 • May 2017 (169)
 • June 2017 (205)
 • July 2017 (190)
 • August 2017 (195)
 • September 2017 (186)
 • October 2017 (235)
 • November 2017 (253)
 • December 2017 (266)
 • 2016
 • January 2016 (165)
 • February 2016 (165)
 • March 2016 (190)
 • April 2016 (143)
 • May 2016 (245)
 • June 2016 (182)
 • July 2016 (271)
 • August 2016 (248)
 • September 2016 (234)
 • October 2016 (191)
 • November 2016 (243)
 • December 2016 (153)
 • 2015
 • January 2015 (1)
 • February 2015 (4)
 • March 2015 (166)
 • April 2015 (108)
 • May 2015 (116)
 • June 2015 (120)
 • July 2015 (148)
 • August 2015 (157)
 • September 2015 (188)
 • October 2015 (169)
 • November 2015 (173)
 • December 2015 (207)
 • 2014
 • March 2014 (2)
 • 2013
 • March 2013 (10)
 • June 2013 (1)
 • 2012
 • March 2012 (7)
 • April 2012 (15)
 • May 2012 (1)
 • July 2012 (1)
 • August 2012 (4)
 • October 2012 (2)
 • November 2012 (2)
 • December 2012 (1)
 • 2011
  2010
  2009
  2008
  2007
  2006
  2005
  2004
  2003
  2002
  2001
  2000
  1999
  1998
  1997
  1996
  1995
  1994
  1993
  1992
  1991
  1990
  1989
  1988
  1987
  1986
  1985
  1984
  1983
  1982
  1981
  1980
  1979
  1978
  1977
  1976
  1975
  1974
  1973
  1972
  1971
  1970
  1969
  1968
  1967
  1966
  1965
  1964
  1963
  1962
  1961
  1960
  1959
  1958
  1957
  1956
  1955
  1954
  1953
  1952
  1951
  1950