Teknolojia Imebadilisha Maisha Pakubwa

By / Published October 30, 2015 | 12:49 pmtechnology

Maisha yangekuwa vipi bila teknolojia? Watu wangekuwa wanaishi vipi katika ulimwengu wa sasa kama hatungekuwa na teknolojia hata kidogo? Siku hizi ulimwengu umebadilika kutokana na mabadiliko katika ulimwengu wa teknolojia japo uvumbuzi bado unatolewa kila uchao.

Naomba tuangazie mawasiliano. Wajua tofauti kubwa kati ya wanadamu na wanyama ni kwamba wanadamu wana uwezo wa kuwasiliana kwa kutumia lugha ambayo huwa pengine kwa njia ya kutumia maneno ama ishara. Dhima kuu ya kuwasiliana baina ya wanadamu ni kuuwasilisha ujumbe na kuhakikisha kuwa ujumbe ambao umekusudiwa kuwasilishwa unawasilishwa kwa njia mwafaka bila mushkil wowote.

Hali hii ya uwezo wa wanadamu kuwasiliana inatupa taswira kamili kuwa ulimwengu haungefikia kiwango ambacho umefikia kwa sasa bila njia mwafaka ya kuwasiliana. Kuna vikwazo mbalimbali ambavyo huwazuia watu kuwasilisha ujumbe kwa njia mwafaka na mojawapo wa kikwazo kikubwa ni utofauti katika matumizi ya lugha. Kila mja ana lugha yake ambayo huwa anaitumia kuwasilisha ujumbe na mara nyingi hali hii hutatiza mawasiliano hasa ikiwa pande zote mbili ambazo zinashiriki katika mazungumzo hazitumii lugha moja.

Kwa mfano, ni vigumu kwa mkenya ambaye anakifahamu Kiswahili tu kuwasiliana kwa njia mwafaka na mja kutoka marekani ambaye kwake lugha ya Kiswahili ni kama usiku wa giza. Hebu fikiria, hapa kuna waja wawili, mmoja anajua tu kuzungumza Kiswahili na kiingereza kwake ni kitendawili na kuna mwingine ametoka marekani na anakifahamu kiingereza tu na Kiswahili kwake ni kama mazigaombwe na jamaaa hawa wanataka kuzungumza na waelewane pengine kwa ajili ya shughuli za kibiashara, je wataweza kuwasiliana vizuri kweli? Bila shaka hataweza kuwasiliana vizuri. Kwa nini? Kwa sababu ya utofauti wa lugha.

Katika hali kama hii, utafsiri unahitajika na watu wengi huanza kumsaka mkalimani. Wakati mwingine kupatikana kwa mkalimani huchukua muda na pia ni ghali kumlipa mkalimani. Mkalimani pia huchukua muda mrefu na hivyo basi kurefusha mazungumzo na hata wakati mwingine maana hupotea na dhima halisi ya kuuwasilisha ujumbe hupotea.

Lakini hakuna haja ya kukuna kichwa tena kwa sababu teknolojia imerahisisha haya yote kwa kukuletea tafsiri ambayo inatafsiri lugha jinsi ilivyo na bila kupoteza maana na hivyo basi kurahisisha mawasiliano, kubadilishana mawazo na hatimaye kuinua uchumi wa taifa na mataifa.

Tafsiri ya Kiswahili ya Microsoft ni teknolojia ya kisasa ambayo inamwezesha mtumiaji wake kupata fursa ya kutafsiri mazungumzo kutoka katika lugha ya kiingereza hadi katika lugha ya Kiswahili ama na kinyume chake pia bila tatizo lolote. Unashangaa kama hili linawezekana? Ewe! Yote yawezekana na tafsiri hii ya Kiswahili ya Microsoft na ni mufti kiasi kwamba kuna uwepo wa mawasiliano ya moja kwa moja kwa kutumia lugha tofauti lakini kila mmoja anapata ujumbe katika lugha ile ambayo anaielewa.

Tuseme kuna mzungu anataka kuwasilaiana na mkenya ambaye anaelewa tu Kiswahili kwa kutumia mtandao wa Skype. Katika hali kama hii, mzungu atatumia kiingereza kuwasilisha ujumbe naye mkenya atapata ujumbe huo katika lugha ya Kiswahili, akishapata ujumbe, atajibu kwa Kiswahili naye mzungu atapata majibu hayo katika lugha ya kiingereza bila maana kupotea na ujumbe kuwasilishwa kwa njia asilia.

Jaribu tafsiri ya Kiswahili ya Microsoft na ujionee, utaipenda na utaishikilia Kikiki.


More Articles From This Author
Trending Stories


Other Related Articles


SOKO DIRECTORY & FINANCIAL GUIDEARCHIVES

2024
 • January 2024 (238)
 • February 2024 (227)
 • March 2024 (190)
 • April 2024 (133)
 • May 2024 (157)
 • June 2024 (145)
 • July 2024 (106)
 • 2023
 • January 2023 (182)
 • February 2023 (203)
 • March 2023 (322)
 • April 2023 (298)
 • May 2023 (268)
 • June 2023 (214)
 • July 2023 (212)
 • August 2023 (257)
 • September 2023 (237)
 • October 2023 (264)
 • November 2023 (286)
 • December 2023 (177)
 • 2022
 • January 2022 (293)
 • February 2022 (329)
 • March 2022 (358)
 • April 2022 (292)
 • May 2022 (271)
 • June 2022 (232)
 • July 2022 (278)
 • August 2022 (253)
 • September 2022 (246)
 • October 2022 (196)
 • November 2022 (232)
 • December 2022 (167)
 • 2021
 • January 2021 (182)
 • February 2021 (227)
 • March 2021 (325)
 • April 2021 (259)
 • May 2021 (285)
 • June 2021 (272)
 • July 2021 (277)
 • August 2021 (232)
 • September 2021 (271)
 • October 2021 (305)
 • November 2021 (364)
 • December 2021 (249)
 • 2020
 • January 2020 (272)
 • February 2020 (310)
 • March 2020 (390)
 • April 2020 (321)
 • May 2020 (335)
 • June 2020 (327)
 • July 2020 (333)
 • August 2020 (276)
 • September 2020 (214)
 • October 2020 (233)
 • November 2020 (242)
 • December 2020 (187)
 • 2019
 • January 2019 (251)
 • February 2019 (215)
 • March 2019 (283)
 • April 2019 (254)
 • May 2019 (269)
 • June 2019 (249)
 • July 2019 (335)
 • August 2019 (293)
 • September 2019 (306)
 • October 2019 (313)
 • November 2019 (362)
 • December 2019 (318)
 • 2018
 • January 2018 (291)
 • February 2018 (213)
 • March 2018 (275)
 • April 2018 (223)
 • May 2018 (235)
 • June 2018 (176)
 • July 2018 (256)
 • August 2018 (247)
 • September 2018 (255)
 • October 2018 (282)
 • November 2018 (282)
 • December 2018 (184)
 • 2017
 • January 2017 (183)
 • February 2017 (194)
 • March 2017 (207)
 • April 2017 (104)
 • May 2017 (169)
 • June 2017 (205)
 • July 2017 (189)
 • August 2017 (195)
 • September 2017 (186)
 • October 2017 (235)
 • November 2017 (253)
 • December 2017 (266)
 • 2016
 • January 2016 (164)
 • February 2016 (165)
 • March 2016 (189)
 • April 2016 (143)
 • May 2016 (245)
 • June 2016 (182)
 • July 2016 (271)
 • August 2016 (247)
 • September 2016 (233)
 • October 2016 (191)
 • November 2016 (243)
 • December 2016 (153)
 • 2015
 • January 2015 (1)
 • February 2015 (4)
 • March 2015 (164)
 • April 2015 (107)
 • May 2015 (116)
 • June 2015 (119)
 • July 2015 (145)
 • August 2015 (157)
 • September 2015 (186)
 • October 2015 (169)
 • November 2015 (173)
 • December 2015 (205)
 • 2014
 • March 2014 (2)
 • 2013
 • March 2013 (10)
 • June 2013 (1)
 • 2012
 • March 2012 (7)
 • April 2012 (15)
 • May 2012 (1)
 • July 2012 (1)
 • August 2012 (4)
 • October 2012 (2)
 • November 2012 (2)
 • December 2012 (1)
 • 2011
  2010
  2009
  2008
  2007
  2006
  2005
  2004
  2003
  2002
  2001
  2000
  1999
  1998
  1997
  1996
  1995
  1994
  1993
  1992
  1991
  1990
  1989
  1988
  1987
  1986
  1985
  1984
  1983
  1982
  1981
  1980
  1979
  1978
  1977
  1976
  1975
  1974
  1973
  1972
  1971
  1970
  1969
  1968
  1967
  1966
  1965
  1964
  1963
  1962
  1961
  1960
  1959
  1958
  1957
  1956
  1955
  1954
  1953
  1952
  1951
  1950